Inashangaza! Kwanini hakuna huduma ya maji ya bomba Mbezi Makabe?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Katika vitu vimenishangaza ni hili, yaani Mbezi pamoja na umaarufu wote huu na kuwekewa hadi Stand Kuu ya mabasi ya kimataifa bado maji safi hayajafika.

Ukizunguka nyuma kidogo ya stendi Mbezi Makabe hatua chache tu watu wanaishi kama vijijini ambako huduma za maji wanajuaga zipo tu mjini.

Cha ajabu zaidi nikionaga uzinduzi wa miradi ya maji vijijini najuaga mijini matatizo yalishaishaga aisee kumbe chenga tu, mbwembwe za kina Kitila Mkumbo miaka yote ya ukatibu mkuu kumbe hata kupeleka maji mbezi tu hapo walishindwa.

Nilishangazwa sana watu wanatumia maji chumvi ya visima miaka yote nikajua maji ya bomba yamekatika kumbe hata kufika hayajafika.
Seriously? Dar? Mbezi? Miaka yote hii? Kweli?

Mweh!
 
Nchi hii ni tajiri, hao ambao hawana maji huko Mbezi wamesema wao hawataki mabomba yao yatoe maji bali maziwa-alisika MATAGA akiropoka kwa sauti.
 
Aisee , Umeandika kwa hasira sana. pole sana mdau.

nadhan maji yamefika ila sio kila sehemu/kila nyumba kama mjini.
 
Dawasa siwamepitisha bomba lao hapo na mara nyingi wanatangaza watu waombe kuunganishiwa maji kwa mkopo watalipa polepole!!!!
 
Poleni sana, serikali italifanyia kazi swala lenu...
 
Ni kweli kuanzia Makabe mpaka Msakuzi hakuna maji ya DAWASA. Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa hawa wenzetu wa DAWASA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…