Inashangaza mnaishia kukagua kwa mama ntilie tu!

Inashangaza mnaishia kukagua kwa mama ntilie tu!

Shujaa Nduna

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2022
Posts
599
Reaction score
487
Ninyi watu wa usafi huwa mnapita kwa mama ntilie kukagua apron kama wamevaa safi, lakini muwe mnatazama na maji wanayooshea vyombo, machafu hata bata hanywi.

Mariam-John-5-1024x640.jpg

Picha kutoka maktaba
Sasa twende katika hoja ya leo. Kwanini watu wa afya hamuwapi elimu na kuwasisitiza wale wanaopakia uchafu kwenye magari wazingatie uvaaji buti, suruali ndefu, gloves na kofia?

Wanashika uchafu kwa mikono, wengine wanavaa raba tu tena nimemuona mwingine anakula yupo kwenye gari ya taka! Chukueni hatua, hamuogopi mlipuko wa magonjwa?

Halmashauri, Manispaa na Jiji muwajibike.
 
Back
Top Bottom