Inashangaza sana mtu analipa hela kuangalia mpira kwenye TV huku bado anasikiliza kwenye redio

Hao watu wamesababisha jamaa yangu a stop kulipa king'amuzi mwezi wa 3 huu ameona angalie mpira kwenye mabanda...maana watu wanamjia ghetto na vi redio wakati wanakuja kutazama kwenye TV
 
mpira unaotangazwa kwenye radio unawahi kupata matokeo kabla wa kwenye TV kwa hiyo mtu anakua na shauku ya kujua nini kinatokea kabla ya kuona kwenye runinga
Huwa naona kama ni upuuzi tu, pia inakera kwa wengine, kwa nn usichague Moja?
 
Hao watu wamesababisha jamaa yangu a stop kulipa king'amuzi mwezi wa 3 huu ameona angalie mpira kwenye mabanda...maana watu wanamjia ghetto na vi redio wakati wanakuja kutazama kwenye TV
Wanakera sana
 
Raha yako inaweza ikawa sio ya mwenzio,ndio maana wengine kuvuta bangi tunapata raha kuliko nyapu.

Kama kusikiliza redio ndio raha yake basi akakae chini ya mti asikilize atuache ambao raha yetu ni kutazama kwenye TV....kila mtu abaki na starehe yake.
 
Hii tabia imekithiri mwanza hua nakwazika sana mimi
 
VITUKO VYA MABANDA YA VIDEO

1. Jamaaa linakuja na redio yake kuna wale wanaoweka headphone lakini kuna wanao fungulia kwa sauti

2. Goli huku hamjaliona jamaa linaanza kushangilia

3. Umekaa kwenye siti yako linakuja lijamaa lirefu linakaa siti ya mbele kabisa yako huoni tena ukiliulinza linaanza ugonvi
 
Kuna hawa wengine wanakuja na runinga kwenye Press Conference......nao sijui vipi[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Yan huwa nikikaa karibu na mtu wa namna hio huwa naondoka,inakera sana
 
Kuna hawa wengine wanakuja na runinga kwenye Press Conference......nao sijui vipi[emoji41][emoji41][emoji41]
Viroba vilivyopigwa marufuku bado vinapatikana mtaani kwenu?
 
Hii tabia nimeishuhudia huku usukumani,

kwa ufupi wasukuma ni Mojawapo ya makabila top three kwa ushamba Tanzania!
 
Kama nina simu ambayo ni kama ofisi yangu kuna haja ya kuwa na saa ya mkononi? Saa ya simu haitoshi?
 

Hii tabia hunikera sana unakuta lijamaa linasikilizia karibu yako yaani mnakuwa mnaangalia marudio kabla hamjaona goli kwenye tv watu wanasimama kushangilia
bora wawe wanasikilizia makwao sio huku vibanda umiza hiyo ni mushkeli kabisa
 
Kuna mzee mmoja huwa ni wa man u ligi ya hapa ni simba anawalamba vyenga huku nje akishika lukaku mpira anavyozungusha miguu sasa hapo chini kuna banda umiza moja halijasakafiwa akienda tu lazma wamwange maji pale chini alipokaa otherwise ile vumbi hamtokaa yani kwenye kiti hatulii ashawahi kumuuma mtu wa mbele yake kisa tu jamaa kakosa goli kwenye tiv anamzuka huyo
 
lugha tatizo hasa kwa game za ulaya.
 
Mpira unaotangazwa una vionjo vya watangazaji na uchambuzi vinavyokoleza starehe.
 
Mashabiki wa mbumbumbu fc ndio wanaoongoza kwa ujinga huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…