Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Yani... Njaa imefanya tunaandikwa vibaya huko mitandaoni.... Hizi ni fursa ambazo tunapaswa kusemwa vizuri na sihivi tulivyosemwa... Tumelia hapa kutaka yule jamaa wa Mambio kuja bongo alafu nyuma ya Pazia tunasumbua watu wanaofanya makala ambazo tungeweza kuzitumia kujitangaza vizuri kwenye majukwaa ya kimataifa... Huzuni kwakweliTatizo kubwa si hawa wageni waliokutana na changamoto mpakani, tatizo kubwa ni mfumo unaowazalisha maafisa wanaoona mgeni kama fursa ya kipato cha haraka badala ya fursa ya kuitangaza nchi.
Nchi nyingi zimejifunza kuwa mipaka yao ndiyo dirisha la kwanza la taswira ya taifa. Mtu akipokelewa vizuri mpakani, tayari nusu ya sifa za nchi zimejengwa. Lakini akikutana na urasimu, vitisho au ishara za rushwa, anabeba simulizi hilo kwenda kulisambaza duniani.
Hawa vijana wa Recharging Hope hawakuwa watalii wa kawaida; walikuwa wanabeba hadithi ya Afrika ya teknolojia ya kijani. Hiyo ilikuwa nafasi ya bure kabisa kwa Tanzania kuonekana kwenye ramani ya ubunifu.
Badala yake, tukawaweka kwenye simulizi ya kusubiri, kubishana na kutiliwa mashaka.
Hii ndiyo tofauti ya mataifa:
Wengine huona mgeni kama balozi wa sifa, sisi mara nyingi tunamwona kama pochi inayotembea.
Mpaka tukibadilisha fikra hii ya muda mfupi, tutabaki tunashangaa kwa nini wawekezaji wanapita karibu nasi lakini hawakai.
Wewe kama unapenda mada za MMU pita kimya kimya watu wachukue madini😏mada yako imekaa kisomi sana
Ndio maana haina wachangiaji
Humu leta mada za mapenz utashangaa uzi unavyopepea
Sio jambo la ajabu kwa nchi yetu kunuka rushwa kwenye hiz boarder wakiona mgen wanajua watapata chochote
Mzee acha kabisa.. ni aibu sana .. nimeshawahi kushuhudia wageni fulani wakipata usumbufu wa kulazimishwa kutoa so called tips . Aibu niliona mimi yaanimada yako imekaa kisomi sana
Ndio maana haina wachangiaji
Humu leta mada za mapenz utashangaa uzi unavyopepea
Sio jambo la ajabu kwa nchi yetu kunuka rushwa kwenye hiz boarder wakiona mgen wanajua watapata chochote
Nilikuwa sijui kama na sisi tuna Tips😂Mzee acha kabisa.. ni aibu sana .. nimeshawahi kushuhudia wageni fulani wakipata usumbufu wa kulazimishwa kutoa so called tips . Aibu niliona mimi yaani
Hivi Mapunga, Tanzania ndio wapi? Kaangalie pale 13:53 inasoma Mapunga, Tanzania Day Ride 4Wakuu, nawasilisha kwa uchungu mno!
Anamaanisha MafingaHivi Mapunga, Tanzania ndio wapi? Kaangalie pale 13:53 inasoma Mapunga, Tanzania Day Ride 4
Mboni wa wenyewe wameandikaWakuu, nawasilisha kwa uchungu mno!
Wamesema Mapunga, Tanzania elewa neno Mapunga, Tanzania unaelewa maana ya Mapunga, Tanzania? Fika mpaka pale dakika ya 13:50 mpaka 56 utaona wamechapa Day Ride 4 Mapunga, Tanzania yeah yeah yeahAnamaanisha Mafinga
Mapunga ipo Zambia sio Tanzania, kwa hio pale producer amekosea kufanya editingAnamaanisha Mafinga
Aina ya watu wenye uwezo ndogo wakufikiri ndio waendeshaji wa mipango mikubwa katika taifa...Kuna mfululizo wa dokumentari nilikuwa naufuatilia unaoonyesha safari ya timu ya Recharging Hope. Hawa ni vijana wabunifu, wanaosafiri kwa pikipiki zinazotumia umeme wa jua (Solar-powered electric motorcycles) kutoka Nairobi kuelekea Cape Town. Lengo lao ni kuonyesha kuwa teknolojia za kijani (Green Tech) zinawezekana Afrika kwa kutimiza azma ya kuendesha pikipiki kwa zaidi ya kilomita 6,000 kupitia nchi sita-Kenya, Tanzania, Malawi, Zambia, Botswana, na Afrika Kusini.
View attachment 3558026
Lakini kama kawaida yetu hapa nyumbani, huwa hatukosagi namna ya kujichafua. Yaani tumejishikiria, wamepita kote huko salama, lakini kimbembe kimeenda kuwakuta mwishoni kabisa mwa ardhi yetu. Hali hii inatia kichefuchefu na inacha maswali mazito juu ya uelekeo wetu kama taifa linalojinasibu kutaka maendeleo:
Urasimu wa Kipumbavu kupata huduma za Mipakani
Katika Episode ya 3, timu ya Recharging Hope imeweka wazi madhila yaliyowakuta mpaka wa Tanzania na Malawi. Wanasema walisota kwa zaidi ya saa nne kutokana na urasimu usio na kichwa wala miguu. Kibaya zaidi, wanakiri kuwa kuna watu walijaribu kuwatapeli (scam) mchana kweupe, jambo lililozua malumbano makali. Hii ni aibu ya kitaifa jamani! Badala ya kuwapokea kwa stara watu wanaotengeneza makala kwa tabasamu na kuwapa kila msaada ili kuitangaza nchi kwenye hizo Makala zao, sisi tunawatazama kama "fursa" ya kupooza njaa zetu na tamaa za muda mfupi.
Tunafukuza "Startups" na Kujichimbia Kaburi la Uwekezaji
Dunia haitusubiri. Startups na makampuni ya teknolojia yanatafuta mazingira ambako akili na muda wao vinaheshimiwa. Ikiwa watu wanapata "stress" ya kijinga na kukumbana na ukasuku wa kishamba wa maafisa wetu, nani mwingine atathubutu kuja akiiona hii Makala? Kwa tabia hizi, tusishangae kuona wawekezaji wakikimbilia nchi jirani ambako mifumo yao imetulia na haina "njaa" ya namna hii.
Tunaharibu Taswira ya Nchi Kimataifa (Reputational Damage)
Video hii inatazamwa na dunia nzima. Jamaa wameipa Title ya "Stopped by ICE in Tanzania???" ni pigo kwa utalii na diplomasia yetu. Inatengeneza taswira ya nchi "iliyooza" (rotted) kuanzia kwenye mifumo ya utoaji huduma. Hata kama tuna mibuyu mizuri na ukarimu wa watu wa vijijini kama jamaa alivyosema, uchafu huu wa maafisa wetu wa mipakani wanafuta mema yote yaliyotangazwa kupitia kwenye hiyo "Royal Tour".
Jamani tuache ushabiki usio na tija. Nchi yetu inahitaji mabadiliko ya kifikra kuanzia ngazi za chini hadi juu. Vinginevyo, tutabaki tunapiga makofi kwa mafanikio ya wenzetu huku sisi tukiishia kuwakamua na kuwakatisha tamaa wageni wachache wanaokuja na mwanga wa matumaini.
Tazama aibu hii hapa:
Stopped by ICE in Tanzania???
Wakuu, nawasilisha kwa uchungu mno!
View attachment 3558027