Inasikitisha mno, hali siyo nzuri kabisa kuhusu wastaafu

Inasikitisha mno, hali siyo nzuri kabisa kuhusu wastaafu

Joined
Jul 19, 2021
Posts
15
Reaction score
52
Benki ya Standard Chartered iliamua kufanya utafiti wa maisha halisi ya wastaafu wapatao 100..

Kutoka kwenye ajira za Serikalini, Mashirika ya Umma na Makampuni binafsi kwa muda wa miaka mitano (5) wakapata na matokeo yafuatayo:

1. Wastaafu 49 kati ya 100 (49%) walikuwa tegemezi kwa ndugu zao na jamaa zao. (walishindwa kujimudu).

2. Wastaafu 29 kati ya 100 (29%) walikufa kwa sababu ya msongo wa mawazo, masononeko na magonjwa ya moyo kutokana na ugumu wa maisha.

3. Wastaafu 12 kati ya 100 (12%) walifilisika na kuishiwa mali zote walizokusanya wakati wakiwa wanafanya kazi.

4. Wastaafu 5 kati 100 (5%) walilazimika kutafuta kazi nyingine za kuajiriwa baada ya kustaafu ili waweze kujikimu na ugumu wa maisha.

5. Wastaafu 4 kati ya 100 (4%) walikuwa na uhuru wa kifedha, waliweza kuyamudu mahitaji yao bila changamoto kwa kuwa waliwekeza.

6. Mstaafu 1 kati ya 100 (1%) alikuwa tajiri kwa kuwa alijiandalia vyanzo vya mapato wakati bado yuko kazini.

49 + 29 + 12+ 5 + 4 + 1 = 100%

Ina maanisha 4% na 1% ndiyo waliokuwa na heri zaidi kati ya 100%.

Hizi takwimu hazifurahishi hata kidogo!

hivyo ni vyema kujifunza kwa walioshindwe na kuchukua hatua mapema ili kuepuka makosa kama haya uzeeni

NB: by the way kama wewe ni miongoni mwa wanaopenda kujifunza kuhusu hisa na kuanza kuwekeza basi click link hapo chini kupata Pdf ya BUREE! Yenye Mwongozo wa kuwekeza kwenye hisa...!

Ndimi
Habakuki Hussen
Contact number
+255676147714

.
 
Mmh wataka kuwapiga tena na wewe wastaafu wajao. UTT au Fuxed account za benki haiwezi kumfaidisha mtu, kwa nchi hizi zenye hyper inflation rate na undtable exchange rate, mchawi ni kufanya self savings na kuwekeza kwenye biashara anazo weza kumudu wakati bado iko kazini, kinacho ua hao wa staafu ni kukopa mara kwa mara benki zenye riba kubwa.
 
Changamoto mfumo wa maisha yalivyo. Unastaafu unawategemez (unasomesha) na kuhudumia familia yenye watu 6/10 means kwamba ata kias utachopat kitaaisha hasa kam hukuw na biashara ukiw kazn
 
Mshika mbili moja humponyoka, ukishika sana shughuli zako za kuajiriwa hutazifanya kwa ufanisi, na kinyume chake pia. Hizo biashara/shughuli utazifanya muda gani wakati muajiri naye anataka ukamfanyie shughuli zake? Itabidi umfanyie muajiri kaza zake na zako uje uzifanye ukiwa umestaafu in the late time umechoka na huna nguvu za kukimbiakimbia huku na kule kutafua fursa za masoko ya bidhaa/shughuli zako
 
Back
Top Bottom