Inasikitisha sana! Lakini ndio imetokea

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Hakika kifo hakina huruma, hakina saa wala notisi.Kilichomtokea mzee huyu leo asubuhi pale Ubungo Bus Terminal kinasikitisha sana. Mzee wa watu, ametoka nyumbani kwake asubuhi na mapema kuelekea kwenye kituo cha mabasi kwenda huko alikokuwa amepanga kuwa mgeni au kureja nyumbani kwake siku ya leo, bila kujua kuwa Mungu amempangia kifo chake leo kabla ya jua kuchomoza. Mzee, huyu ambaye hakutambulika mara moja, amegongwa na basi la abiria liendalo mikoani wakati likitoka lango kuu kwenda na safari zake, tairi lilipanda mwilini mwa mzee huyu na kumuua hapohapo akiwa ameshika mkoba wake wa safari mkononi. Hivi sasa tunavyosoma habari hii ya kusikitisha mwili wake uko mochwari katika hospitali ya Mwananyamala na kwa yeyote anayemfahamu ajitokeze, nahisi familia yake haina taarifa. Mungu alitoa na YEYE ametwaa mja wake, YEYE ndiye Mfalme wa Mbingu na Ardhi na KWAKE sote tutarejea!! Ailaze roho ya Marehemu Peponi - ameen!
umati wa wasafiri na wapita njia wakishuhudia mzee wa watu akiwa hana kauli tena
...basi la kushoto (ambalo halikuweza kujulikana mara moja) ndilo lililohusika na ajali hiyo. Dereva wake alijisalimisha mikononi mwa polisi, ingawa basi liliruhusiwa kuendelea na safari zake.
..askari polisi wakisaidiana na raia kumpakia marehemu garini



...maiti ikipelekwa kuhifadhiwa Mwananyamala hospitali.

PICHA: Mpiga Picha Wetu. chanzo INASIKITISHA SANA! - Global Publishers

Mwenyeezi mungu muweke Pema peponi kiumbe huy mzee wa watu wana J.F Semeni ameen
 
Da jamani, kweli inasikitisha mno. Imeniuma mno. Poleni wafiwa kwa kuondokewa na mzee wenu. Angalizo, pale bus terminal mabasi yanatoka kwa kasi sana kuingia barabarani tena kwa utemi mkubwa mno. Imefika wakati sasa traffic awe anasimama pale kuhakikisha anasimamisha magari mengine ili mabasi yale yatoke, na pia kuhakikisha watembea kwa miguu wanapita pale kwa usalama.
 
May God Rest his soul in Peace..
I hope ndugu watampata...
 
<!-- google_ad_section_start(weight=ignore) -->Mathayo Chapter 21 42. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

43.
Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. ( Taifa la Kiaarabu ndilo alilolitabiri Bwana Yesu Taifa lenye kuzaaa Matunda yake Wayahudi hawakumuamini bwana Yesu Mungu awapa waarabu Taifa la wenye kuzaaa Matunda)
[FONT=Trebuchet MS, Arial, Helvetica]

kwa hiyo kumbe waarabu ni wakristo na uislam ni dhehebu ndani ya ukristo?kama wayahudi hawakumwamini na waarabu wakamwamini ndio wamekuwa wafuasi wake na ndi o aliotaka wabatizwe kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu. bwan yesu asifiwe sana shehe wangu.nikukumbushe vilevile imeandikwa hapohapo kuwa ila kinywa kitakiri yesu ni bwana.peleka ujumbe huu msikitini.
[/FONT]
 

Inasikitisha sana. RIP

(Naona hapo juu kuna bango la mtu wa watu)
 
Asante mdau kwa taarifa ya kusikitisha.Ila sijaelewa unaposema"........basi hilo hapo kushoto ambalo halikuweza kufahamika mara moja....!!!wakati basi linaonekana na mtoa habari uliliona physically!!!sema tu hukutaka kulitaja ile kiutu uzima
 

Hii inaendana na hii thread kweli?
 
Kifo hakipigi hodi kwa kweli...
Mungu amlaze mahali pema peponi ....... AMEN

(MABONGO YA MTU WATU MWAKA HUU YAMETAPAKAA KULIKO MWAKA 2005, KULIKONI????......WANA-JF MMESHALIGUNDUA HILO????)



Inasikitisha sana. RIP

(Naona hapo juu kuna bango la mtu wa watu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…