Inasikitisha sana pumzika kwa amani Pastory(shabiki wa simba)

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Posts
10,518
Reaction score
13,144


Stori ilikuwa hivi; ndani ya "kibanda umiza" mechi ya derby jana kati ya Simba SC na Yanga SC wakati wa mikwaju ya penati alipoenda kupiga Haruna Niyonzima, Shabiki wa yanga akamwambia shabiki huyu wa simba ; "huyu hapati hii penati ametokea kwetu Yanga" Pastory akamjibu " anapata usibishe"

Niyonzima akazamisha nyavuni ule mkwaju wa penati kwa pigo zuri tu. Pastory wa simba ile furaha akapata mshituko akapoteza fahamu na kukimbizwa hospitali lakini hakuweza kuamka tena. Kutokana na ile furaha ndio ikawa mwisho wa uhai wake Rest in Peace Pastory Kigia (43yrs) Morogoro(Kilombero). Hakika kazi ya Mungu haina makosa lakini ndugu zangu wapenda soka tuwe na kiasi katika mapenzi yetu katika mchezo huu pia lolote lile la kidunia.

Ni vyema zaidi kiimani kumpenda Mungu kuliko jambo lolote . Haya mambo ya watu kufariki viwanjani na katika mabishano ya kisoka yameanza kukua kwa kasi sana sasa hivi pia watu kuzimia viwanjani.

Kabla ya jambo lolote likiwepo hili la kuupenda mchezo huu ni lazima kumweka Mungu mbele akupe ustahimilivu ili uwe na yamini pia kiasi .

Hakuna aijuaye njia yake ya kuondoka humu ulimwenguni lakini tujikite zaidi kwa mapenzi ya asilimia 100/100 katika masuala ya kiimani zaidi pia tujijenge kukubali matokeo ya aina zote katika soka

Pole wana msimbazi wote , familia ya bwana Pastory , wapenda soka na wote tulioguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine.

-Ndumilakuwili-
 
RIP Pastory!!! Mbele yetu Nyuma yako!!!!
Mapenzi yako kwa Club yetu ya Simba Tutayaenzi Daima!!!!
Lala Salama Pastory!!!![emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Duhh...[emoji15] [emoji15]
Mdomo wangu umebaki wazi..[emoji47] [emoji47]
 
Duh r.I.p kwahiyo hata hakuona kua ile ngao iliandikwa sheild?
 
Alikua na matatizo mengine sidhani kama ni goli ndio sababu ya huo mahtuko wa kumuua
 
Alikua na matatizo mengine sidhani kama ni goli ndio sababu ya huo mahtuko wa kumuua
Tatizo Simba waliwajengea matumaini mskubwa sana mashabiki wao kuwa wataifunga Yanga bao nyingi. Kutokana na Usajili waliofanya. Matokeo mambo yameenda kinyume. RIP shabiki wa Simba;
 
Sijawahi elewa ushabiki wa namna hii. Rip kwake!
 
Pumzika kwa Amani Mtani wangu kipenzi - Nakupenda kwa kuwa ulikuwa sehemu ya familia ya Utani wa Jadi.

Tutakufuata na sisi.
 
R I P Pastory, mapenzi ya mungu yatimizwe, wewe ni shujaa na umekufa kishujaa. cha msingi hukujiua, mapenzi uliyokuwa nayo kwa timu yako yameondoa uhai wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…