Jamani kwenye inchi liyotarabika na kwa nafasi walizonazo wa wajumbe wa bunge la katiba sikutegemea lugha na kauli zinazotolewa kwa sasa ! linavyoendelea tunaweza kushuhudia mapingano au kung'oana meno bila ganzi kwa wajumbe kwani lugha zinazotolewa bila kudhibitiwa hazivumiki? Nawashauri wa wajumbe na kuwakumbusha dhamana waliopewa na macho ya watanzania wote yanawatanzama wao .Wasipotimiza wajibu wao wakaleta ushabiki wa kisiasa (watawala na wapinzania) hawataleta katiba itakayoleta mabadiliko ya kweli kwa maisha halisi ya watanzania. wakumbuke wamepata nafasi kuleta mabadiliko kwa amani wasipofanya kama wananchi wanavyotaka wanachi watafanya madiliko wenyewe na vilevile wao sio mwisho wananchi tunayonafasi kuipigia kura katiba ambayo haitakuwa ya wazi wala siri kama wanavyovutana. Hatuwezi kugharamia watu wasiotuletea katiba tunayoitaka matumaini yetu wako mikononi mwao lakini wanayofanya kwa sasa hayawezi kuetenda na mtu mzima aliyestarabika na wasipotimiza wajibu wao WATAWAJIBIKA MBELE YA MWENYEZI MUNGU NA HITORIA , mwl.Nyerere na Sokoine watakakuwa mashahidi