Inasikitisha: Wanakwaya 20 wafariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni

Inasikitisha: Wanakwaya 20 wafariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
13,149
Reaction score
6,994
Kamanda wa Polisi Kaunti ndogo ya Mashariki,Kenya Joseph Yakan alithibitisha kisa hicho, na kuongeza kuwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini.

Katika video,jana jumamosi dec 4,2021,basi hilo lilijaribu kupita daraja lililofurika maji kwa usaidizi wa wakazi.

Baada ya dakika chache,basi hilo lilionekana likihangaika kusogeza magurudumu yake kwa vile mawimbi ya maji yalikuwa makali sana hivyo kulipeleka mtoni.

Waumini wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini.

Bus lilikuwa na takrabani watu 30,ajali ilipotokea saa moja asubuhi katika kijiji cha Ngune,Mwingi ya kati.
 
Hao hapo
 
Mbona wanaonekana watu kukatiza hapo hapo basi liliposhindwa na hawaonyeshi kupelekwa na maji............imagine uzito wa basi na mtu, nilitarajia watu waliokatiza hapo nao wangekokotwa na maji, anyway RIP.
 
Kwa sababu ambazo ni dhahiri, chombo cha habari au binadamu mwenye busara hawezi kuonyesha tukio lote mpaka mwisho. Kimaadili na pia kibinadamu siyo vizuri na haingii akilini. Hata kama ni mtu mwenye busara anarekodi tukio kama hilo, ataacha mara itakapofikia hatua kama hiyo.
 
Kila nafsi itaonja Umauti,Wapumzike kwa Amani Wana Kwaya wote.
 
Uzembe wa dreva na uzembe wa viongozi kushindwa kujenga miundombinu bora umechangia ajali hio kutokea
 
Mbona wanaonekana watu kukatiza hapo hapo basi liliposhindwa na hawaonyeshi kupelekwa na maji............imagine uzito wa basi na mtu, nilitarajia watu waliokatiza hapo nao wangekokotwa na maji, anyway RIP.
Chasis iliyokosa viwango! Barabara ya Lamu port hii!
 
Back
Top Bottom