BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Inatosha: Academy zinatumia Kiingereza kutuzuga
Daily News; Tuesday,September 16, 2008 @15:55
Wakati akiwa Babati mkoani Manyara siku chache zilizopita, Rais Jakaya Kikwete aliwabeza wanafunzi wa shule moja inayofundisha kwa Kiingereza ambao walimwimbia nyimbo za kwaya kwa Kiingereza na Kifaransa na alipowauliza kwa nini hawakuimba kwa Kiswahili wakamjibu kwa kimombo kuwa We do not know Swahili, wakimaanisha kwamba hawafahamu lugha hii ya taifa.
Kwa kumnukuu Rais Kikwete, ingawa Kiingereza ndiyo lugha muhimu duniani Kiswahili kina nafasi ya pekee nchini kwani ndiyo lugha ya taifa na hakipaswi kudharauliwa.
Alichokisema Rais Kikwete Babati kinaibua upya mjadala wa umuhimu wa lugha hizi mbili Kiingereza na Kiswahili katika kufundishia masomo ya shule za msingi na sekondari nchini, hasa katika zile zinazofahamika kama Academy.
Kwa jinsi hali ilivyo sifa moja kubwa ya Academy hizo ni umahiri wao wa kuwawezesha wanafunzi wake kuwa na uwezo wa kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha tangu madarasa ya chini.
Sisi hatupingi wazo la kutoa uzito wa pekee katika matumizi ya Kiingereza kwenye shule hizo kwani ndiyo lugha inayohitajika baadaye katika kujifunza taaluma nyingine kama udaktari au uhandisi.
Kinachotupa tashwishwi ni namna Kiingereza kinavyopewa kipaumbele katika Academy kana kwamba ndilo somo pekee linaloweza kumfanya mwanafunzi awe mwanataaluma bora. Kiswahili na masomo mengine yanapewa uzito mdogo au yanawekwa kando.
Hata hivyo, ukweli ni kwamba dunia tuliyoko sasa ni ya sayansi na teknolojia na kwa sababu hiyo tulitarajia kwamba Academy zingekuwa za mfano katika kutoa kipaumbele kwa masomo kama Hisabati na Sayansi badala ya Kiingereza pekee.
Tunadhani wakati umefika sasa kwa Academy na shule nyingine pia kuwa chemichem ya wanasayansi wetu wajao kwa kuwaandaa kwa umahiri kama zilizofanikiwa katika lugha ya Kiingereza. Zikichelea kubadilika zitatuandalia taifa la kesho ambalo linaweza kuwa na mamilioni ya wazungumza kimombo lakini wasio na weledi katika taaluma nyingine yoyote.