Inatosha sasa, wanachuo tuchukue hatua

luvafrica

Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
56
Reaction score
20
Habar zenu wanajamii wenzangu,

Naimani muwazima wa afya, kwa upande wangu namshukuru Muumba kwa neema ya uzima. Kichwa cha mada kihusike kwa walengwa wote, hapa nawaongelea sana sana graduates. Ni jambo la kawaida sana kukutana na vijana wengi tu mtaani wasio na ajira maalumu au kazi ya kufanya tena kwa miaka kadhaa kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira za kutumia vyeti, naongelea ajira za maofisini.

Samahan naomba msinielewe vibaya, sina maana ya kuponda wanaohangaikia ajira miaka kadhaa na kuendelea kuilaumu system au serikali bali nataka tujuzane alternatives zingine za kufanya ili tuweze kufit sehemu tunazostahili. Kwa lugha nyepesi naomba kupitia uzi huu tujuzane njia za kupitia/kufanya hasa tukiwa bado masomoni ili pale tunapohitimu elimu zetu tujue tunaanzia wapi sio tunarudi home mikono kichwani tukiwaangalia wazazi/walezi wetu huku nao pia wakipay attention kujua ni kipi kipya tumerudi nacho.

Kwa kuanzia natoa views zangu halafu nitaomba tuchangie pia mitazamo yenu ili tuweze kusaidiana maana haipendezi hata kidogo mtu unapita mtaani watu wanakunyoshea vidole, utasikia umemwona yule mkaka mwenye bahasha ya kaki,! toka kamaliza chuo mwaka juzi hana analofanya zaidi ya kupiga stori na mlinzi wa mama Semeni!

Duuuh Nionavyo mimi chuo/shule ni taasisi muhimu ambayo ukitumia akili yako vizuri ni rahisi kutambua au kujifunza jinsi ya kugundua fursa za kiuchumi maeneo mbalimbali. Maana yangu ni kuwa unaweza kubadilishana ujuzi na wenzio mfano kwa kuulizia mnafanya nini wenzangu ukiachalia mbali kitabu?

Ukiwa serious na willingly hapa utapata kitu. Pia mavyuoni siku hizi huwa kuna semina kibao za ujasiriamali, tia mguu huko. Mbali na hayo yote kuna kina Thomas na Ngina ambao bodi ya mikopo inawatambua, wapendwa tujaribu kujiwekea akiba kutoka kwenye hicho kidogo tukipatacho na kisha kukitumia baadae kama kimtaji. Nina mfano wa wadau wengi tu ambao wametoka kupitia hii njia. Kuna slogan mtaani inasema CHANGES BEGIN WITH YOU, haya basi kila mmoja wetu ashike panga na shoka tayari kwa kutokomeza janga la ajira kwa wasomi. Twende pamoja kwa kutoa michango positive mfano kwa kutoa mifano halisi ya watu waliootoka bila kutegemea ajira.

MUBARIKIWE..
 
Hlo kweli kabisa wakati mwingine ni maumivu wanayopata wazazi/walezi wetu make lengo la mzazi/mlezi yeyote ni kumwona mwanae akinufaika na kupata kazi kutokana na kazi walofanya kukusomesha
 
Kweli mkuu wil, wazazi huwa hawatumalizi ila ndo ivo system ya elimu ya tz nayo ni kikwazo,lakin hatujachelewa tuna chance ya kuibadili maana mabadiliko inabd yaanze na mtu mmojammoja
 
Sa nyingine tuihurumie serikali sio kila kitu tunalaumu serikali na kuifananisha na nyingine wakati serikali zina uwezo tofauti.

Mi nashauri kila mtu atumie akili yake na ubunifu wake kujitafutia kipato na si kuilaumu serikali kwa sababu tumekuwa mzigo mzito kwa serikali.
 
Source of capital zipo nyingi tu.unaweza kuanzisha biashara hata ndogo tu,sema wanachuo wengi wanajifanya matawi na ubisho.unalalamika mtaji wakati una simu ya laki nane kwa wengine mtaji tosha kabisa

sasa mkuu, chukulia hyo cmu y laki nane cna na mtaji cna na nataka maendeleo nafanyaje hapo!ni lazma serikali ihucike kama ambavyo wanatoa mikopo kabla ya chuo bac wafanye vivyohivyo baada y kumaliza kwa wale watakao kosa kazi.
 
Source of capital zipo nyingi tu.unaweza kuanzisha biashara hata ndogo tu,sema wanachuo wengi wanajifanya matawi na ubisho.unalalamika mtaji wakati una simu ya laki nane kwa wengine mtaji tosha kabisa


Hapa umegusa penyewe mkuu, kipindi hatuja graduate ukimuuliza mtu kuwa ukipata chance ya kupata capital ungependa kufanya biashara gani?

Majibu yao utacheka mkuu, utasikia Mara ohhh napenda niwe na boutique langu niwe nafuata mzigo Dubai, Yaani dreams zao ukiwasikia waweza kuzimia hakuna anayewaza hata kufanya biashara ndogo ndogo ili mtaji ukikua awekeze pakubwa!

Masikini sa hivi sijui hata wapo wapi!
 
Me ntatoa mawazn yangu kidogo maisha kwanza n4 kupgana na kua na nia ya dhati pia uthubutu.

kiukwel kwa wale ambao wanaanza mwaka wa kwanza familia nying huwa na kihoro horo hivyo ujitahid sana kuwapa vijana wao pesa ya matumizi madogo madogo angalau laki kwa miezi 2.

Hivyo kwa watu wenye malengo mnaweza kuunganisha nguvu mkachanga mkanunua boda boda ambayo kwa bei ya mtaani boxer iliyotumika kidogo unaweza kupata ata kwa milion na laki 3 had 5.

Mkinunua mnampa mtu hesabu kwa siku elfu 10 hapo service juu yenu inamana kwa mwezi mna uhakika wa kupata laki 3.

Inamana mpaka semester 1 inaisha miez 3 mtakua mna laki 9 ukitoa na ela ya service mnaweza kubakiwa na laki 7 na nusu.

iyo tayar ni ela nyingi inayoweza kuwapa dira ya kufanya vitu vingine kwa mtaji kidogo mlionao.
cha msingi ni kujituma na kuthubutu.
 

thanks,imeingia akilini#von tosy
 
Vijana wengi tunapenda maisha ya juu yasiyoendana hata na hadhi zetu,simu tunazomiliki tu msemo wa jamaa ni mtaji tosha,maisha ya kuiga yanatuponza pia.

Mfano pesa ya boom huwa inatosha kabisa kwa muda ulopangwa na kwa wenye kujitambua huweka hadi akiba ya kutosha lakini wengi wetu tunaishia kuendekeza starehe.

Back to the UZI suala la ajira,vijana wengi tunapenda kazi kubwa kubwa tu za maofisini....suala la kujiajiri hilo wazo waya wake ulishaoza kabisaa akilini mwetu,kuna njia nyingi sana japo wawezao ni wachache,unaweza kuanza kwa kujitolea sehemu fulan endapo utapata na hii huweza kukupa ajira ya kudumu kutokana na utendaji kazi wako.

Pia suala la kuchagua kazi nalo tuliondoe mfumo wa sasa hauruhusu,lima hata bustani ya mchicha na degree yako hyo mafanikio yaanza kidogo kidogo.
 
Wengi wetu graduates tunapenda mauzo, usharo na udada duu...
Kuna jamaa nipo nae hapa church, actually yeye ndio ameniinspire nizame kwenye biashara, mpk ikafika state nikawa na hulka za kupostpone masomo... but always fortune favours the bold, saivi nina capital ya kutosha na turnover safi saaana...

Huyu bw. alimaliza UDBS 2007, kasanda kitaa karibia miezi6, bahati mbaya home kwao si wasomi wala hawajui system inaendaje, wao wanajua ukimaliza chuo kazi unapata the next day, basi yule bw akaanzishiwa ligi la kufa mtu pale kwao, matusi na masimango non-stop...

Jamaa akaamua avae ngozi ya simba jike, kaingia kitaa kutafuta pesa kwa jasho na damu. Mshkaji akapata wazo la kupiga debe, akaset plan ya kupiga debe ya kidigrii digrii, asubui gari 20 jioni gari 20 only 2 hrs a day, kwa siku alikua anapiga ef20... kapiga nonstop mwezi mzima, akavuna laki6 net.

Akaacha kupiga debe akakamata fursa nyingine, safari hii aliamua ajilipue na biz ya mkaa, by that time gunia lilikua 25'000 on wholesale na anauza 30'000 on retail, jamaa alipiga kwa miezi kama8 then akawa na mtaji mnene kidogo. Akaswitch kwenye kazi ya umiddleman, anachukua mzigo wa viazi mbeya+njombe then analeta masokoni(buguruni, ilala, kisutu, TMK nk) kapiga umiddleman wa kuku(broilers) anachukua kwa wafugaji then anawamwaga sokoni...

Huyu bw tangu 2012 kaingia kwenye biz ya animal feeds, ambapo company yake imeingia top100 midsiezed intreprises in TZ 2014...
There he went, there he prospered....

My take...
Ukimaliza chuo, kamata vyeti ingiza kwenye bahata, dumbukiza kwenye kabati, tia lock... then ingia mtaani mzima mzima, usipepese macho wala usipindishe ambitions zako.
 
Mkuu ontario pokea like kwa mchango wako, graduates tuache kuchagua kazi,eric shigongo ashawahi sema ukiona kazi kufanya shughuli unazohis znashusha hadhi yako basi nenda mbali na eneo lako kafanye shughuli hizo.

Jaman kukosa mtaji ni kigezo kidogo sana mana unaweza kutoka hata bila mtaji kuhusika
 
Hadith yako mzur xana im£tufundixha m£ng kama vp tul£t££ nyingn£
 
Kuna kitu kaongelea mkuu sir jj naomba kuongezea experience yangu kdg, jamaa kasema wanachuo wengi wanapenda urahisi wa maisha sana kiasi cha kutumia boom lake lote kujenga shavu mpk mtu anasahau kujiwekea kiakiba.

Ukiwa na malengo kwa wenye bum lazima utatoka kupitia pesa hiyo!naomba niwaongelee wanafunzi wa udsm as an example, utakuta mtu anatokea katika familia ya kawaida tu lakini nguo hafui yeye anapeleka dry cleaner,mbali na hilo unakuta pesa yake nyingi anatumia kununua vitu kama maji mpk makopo matatu ya sh.600 kwa siku wakati angeweza kununua jagi kwa ajili ya kuchemsha maji ya kunywa kwani pale maji yake hayana chumvi na pia wanafunzi wanaruhusiwa kutumia umeme kwa uhuru zaidi.
 

Ahsante wazo lako ntaenda kuli2mia udom ata kama maji ya chumv ntanunua jag la elfu 35
Marufuku kununua maji ntachemsha
Ahsante sana mkuu luvafrica
 
Last edited by a moderator:
Hiyo mbinu inasaidia mkuu von, sio lazima mtu upende kuishi maisha ya kifahari wakati kipato hakiruhusu.

Ni bora uishi kama mtumwa for good yaani badae unakuja kuishi vizuri,narudia tena kwa msisitizo kuna watu wana maduka makubwa tu,na miradi mingine mingine kibao kwa kutumia pesa ya mkopo mfano kuna jamaa alimaliza mwaka jana ana mashine za kukoboa na kusaga huko moro, dada mmoja pia alimaliza mwaka jana, unaambiwa alinunua bodaboda zake mbili pia mshikaji wangu mwingine alianzia kuuza nguo za ndani na vipodozi mwaka wa kwanza,sahz ni yeye na biashara tena anavuka boda kabisa mara congo, mara zambia na sahz ana plani za kuanza kwenda nairobee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…