SoC01 Inatupasa kuwa na marafiki wenye tija

SoC01 Inatupasa kuwa na marafiki wenye tija

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
habari yako ewe mfuatiliaji wa makala hii,

Karibu kuungana nami ili tupate kujua na kujadili kwa namna gani natupasa kuwa na marafiki wenye tija katika maisha yetu ya kila siku
Ambapo hao marafiki wazuri wanaweza kutusaidia kutatua changamoto mbalimbalu za kimaisha na kutupa ushauri na miongozo bora inayolenga maisha yetu

Na kutupitisha njia watakazoziona zinafaa
Kuna mtu nimewahi kumsikia akisema kwamba sisi vijana tunayo nafasi nzuri sana ya kuwa na maendeleo kwa kuwa karibu na wale walioendelea au wenye mafanikio.

ikiwa na maana kwamba Kwasababu hii itarahisisha wewe kufanikiwa kwa kudokezwa kujikita kwenye fursa zinazokuwa zinajitokeza na hata pia ukajifunza kitu kutoka kwake ambacho pengine kinaweza kuja kukusaidia mbeleni.

Nimeona kwamba kuna haja ya kuongelea hili swala ili pia tuzidi kutanua wigo wa kufahamiana na watu wanaojuana na watu. Maana yake kaa na watu wenye kufahamika kwa wengine na hii ndiyo njia rahisi ya kupata fursa za unachokitafuta au kupata wateja katika biashara yako.

Ili kupata fursa mbalimbali za kimaisha
Tunatakiwa kuchangamana na watu kwa sababu fursa hazikutafuti bali zinatafutwa pia kumbuka ili uweze kufanikiwa unatakiwa kuepuka umimi au ubinafsi kumbuka ya kwamba umoja ni nguvu na pia kama wasemavyo kwamba kidole kimoja hakivunji chawa.

Na pia Jitahidi kuwa mtu katika watu ili watu wakutambue kupitia shughuli uifanyayo Weka heshima kwa kila mmoja bila kujali umri wala hali za watu kwa kuwa hakuna aijuae kesho italeta nini! inapaswa tuelewe kwamba maisha yanabadilika na hayatabiriki

Tunapaswa kufahamiana na watu wanaojulikana kwa watu zaidi. Kwa sababu mafanikio ya siku hizi yanategemea muunganiko yaani (connection) za watu ili kupeana fursa mbalimbali zinazokuwa zinajitokeza.

Nadhani inawezekana wapo ambao huenda tuliwadharau kipindi cha nyuma na kuona si chochote lakini hivi sasa unaweza kushangaa kwa kuona ndiyo wenye maisha mazuri kuliko vile sisi tulivyo

Fahamiana na watu upate fursa mbalimbali kwa maana wao huifungua milango ya fursa mbalimbali, jichanganye na kamwe usibweteke kwasababu haya maisha yanahitaji upigane na ushindi upatikane, Na unatakiwa uibuke mshindi.

Siri kubwa ni kwamba tuwe wavumilivu na tusiyokata tamaa kirahisi naamini tukifanya hivi tutafika mbali.

#je nini wazo lako katika hili, karibu tulijadili.
Asante
 
Upvote 0
Back
Top Bottom