Inauma sana wakuu, kijana amenikata ngwala hadharani

Inauma sana wakuu, kijana amenikata ngwala hadharani

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Kwanza naomba niwaonye wakubwa wenzangu, ili kurahisisha maisha kuna wakati tunapaswa kupuuza baadhi ya mambo ili tujifanyie wepesi.

Naomba nifupishe simulizi.

Leo nilifunga safari kwenda shule fulani kutoa discipline kwa kijana huku nikiwa nimeambatana na fungu moja la bakora (vijana wanaita mzigo wa kuni).

Kama kawaida nikifika shuleni na nikapokewa mfuko wangu nilio bebea nguo zangu, na ule mzigo mwingine kama mnakumbuka watoto pia wakauopokea huku wakishangilia na sikuuona tena (kumbe walizipeleka zile fimbo jikoni na kusema kwamba baba yake na fulani katuletea na zawadi ya kuni).

Basi nikapitiliza hadi ofisi ya mkuu pale, nilipo ingia na kijana akawa amefika tayari maana kidogo pale shule wanafunzi wapo so active kuhabarishana taarifa.

Bila kuchelewa nikaanza kutoa mashtaka yangu mbele ya mkuu pale sasa kijana alipo sikia nikamuona kama anasimama na akataka kukimbia, basi nikataka kumkata ngwala na nikakosea nika kanyaga kamba ya kiatu kumbe nilisahau kuifunga vizuri, wakuu nilikula mweleka right on front of my son.

Hapa nilisimama na nikaanza kujipangusa, basi kijana akasogea na kunipa pole, mzee nikaona usintanie badala ya kuitikia nikanyenyua teke na akalikwepa nikapita na stuli ya ugoko dahhhh.

Hapa ikabidi kijana akimbie nje, na mimi nikaona isiwe tabu maana bado sijazeeka sana, wacha nimkimbize, kijana alinikata chenga mbele ya kundi la wanafunzi katika kumkimbiza wakuu... Nilikula mweleka na nikaangukia upande wa kitambi hadi kidogo suruali ya kaunda niliovaa ikatatuka kwa nyuma kidogo.

Wakuu, kwa leo naomba niishie hapa, haya mambo ya kuwafuatilia vijana wenye damu inachemka zaidi sio sawa, kuanzia Leo nimejifunza na ninawashauri wazee wenzangu kwamba hakuna jambo jema kama mzazi kuongea na mwanae katika kila jambo pasipo kujalisha ugumu ama uzito wa situation husika, na wazazi tupunguze matumizi ya nguvu iliyopita kiasi katika kuwa nyoosha vijana wetu.

Mungu awabariki sana, mimi na familia yangu tunawatakia usiku mwema na amani tele.
 
Back
Top Bottom