Uchaguzi 2020 Inaumiza familia, inaumiza wasiohusika

Uchaguzi 2020 Inaumiza familia, inaumiza wasiohusika

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Tarehe 28/10/2020 umeoga asubuhi na mapema kwenda kuratibu au kusimamia uchaguzi, kwa mazingira yalivyo mkeo na watoto wanakuombea uende na urudi salama huku wakikuomba ukatende haki.

Unafika kazini unaacha kiapo ulichokula cha kulinda Wananchi unaamua au unalazimishwa kudhulumu haki ya wananchi huku ukijiaminisha kwamba upo salama na wanao wapo salama.

Kwa bahati mbaya kitendo ulichokifanya kinaibua Wananchi kudai haki yao na katika kuwatuliza baadhi wanaumia na wengine wanapoteza uhai.

Muda wako wa kazi unaisha unarudi nyumbani, wanao na mkeo wakiwa wanaangalia TV wanaona kilichotokea katika eneo lako na wanapata habari ya madhara yaliyotokea. Unaporudi ndani wanakupokea ila unagundua awana amani. Nafsi inaukumbusha ubongo yaliyotokea, unaanza kujuta, familia inakuona kama mtoa roho.

Tume imedhibiti matumizi ya simu kwenye eneo la uchaguzi, wewe kama boss na mlinzi wa amani ulikua na ruhusa yakutumia simu ila ulikua busy kuwasiliana na wakubwa zako kuhusu njama zao zakudhulumu haki.

Ukiwa chumbani unakumbuka kuwapigia kijijini kwenu, simu ya wazazi wako hazipokelewi. Unapiga kwa ndugu zako wengine unashangaa wanakupa pole kwamba wadogo zako wawili ni baadhi ya watu waliopoteza maisha kutokana na vurugu za uchaguzi, unaanguka unaparalize, kazi wanakuachisha nakukulipa mafao yako baada ya miaka miwili.

Watu mliopewa dhamana kumbukeni damu inaweza lilia familia zenu msiposimamia haki.
 
Na ndivyo inaenda tokea hao wahusika wasipotenda haki.

Haki
Haki
Haki

Kila sikio lisike neno haki linavyotakiwa na Watanzania wengi ili iwepo amani ya kweli kwa Watanzania wote.

Mungu ubariki uchaguzi mkuu wa Tanzania 28/10/2020.

Mungu wape hekima wale wote wanaotakiwa kutenda haki.

Mungu wape Watanzania wote afya njema ya akili,mwili na roho wakachague viongozi wao.

Mungu wabariki Watanzania wote wanaolitakia taifa mema.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Upinzani bhana 😂😂😂 yn nyie n kulalamika tuu mkidhan mnaonewa
 
Kwanini mna hisia za kutotendewa haki?. Chama cha Mbowe hakina kura za kuibiwa, chama kilichokataliwa na wananchi wengi. Na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Genge lenu la wahuni, halina nafasi hapa nchi, Watanzania wote wanakwenda na Mzalendo namba 1 JPM.
 
Back
Top Bottom