only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,527
...Wiki iliyopita kumetokea mahuaji ambayo kila mtanzania mpenda haki na mzalendo atakuwa ameguswa sana na vifo hivi...Ni vifo vya watanzania wenzetu wachumiaji juani kama sisi walipopoteza uhai baada ya kuitwa ni majambazi wa mali za wawekezaji ktk mgodi wa dhahabu kule Musoma....Napata shida kidogo ni nani jambazi kati ya hawa wawekezaji+serikali au wakazi wa Nyamongo...Nilizidi kuumia sana pale nilipomsikia waziri mmoja akisema wale hawakuwa wananchi bali majambazi,na kushangaza serikali hiyohiyo ikapeleka rambirambi kwa wafiwa,nawapongeza wafiwa kwa kukataa unafiki na udhalilishaji huu wa hawa wahuni...Nacho jiuliza
- Je,mpaka lini mali zetu zitakuwa chanzo cha kutoa uhai wetu?
- Je,ni nani jambazi kati ya serikali ya CCM au Wananchi wa Nyamongo?
- Ni nini suluhisho la matatizo haya katika sekta ya madini?
- Je,kuna haja kuwa na serikali isiyowajibika kulinda mali na uhai wa wananchi wake badala yake inakuwa ni kibaraka wa wawekezaji mabeberu?