Inawezekana kabisa Simba SC ikaweza kufuzu mapema robo fainali ugenini

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kinara wa kundi D' akiwa na alama (7) kibindoni, Mnyama Mkali Mwituni Simba SC leo March 20, 2022 anashuka kwenye Dimba la Stade de I'Amitie Cotonou Benin kukiwasha na ASEC Mimosas kwenye mchezo wa marudiano hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Ni mechi ngumu kwa timu zote mbili, ASEC Mimosas ni mwenyeji kikanuni lakini kimazingira ni mgeni kama Simba SC, ambapo wote wanacheza ardhi ya ugenini Nchini Benin.

Simba SC inawezekana kabisa kufuzu robo fainali mapema ugenini endapo Kocha Pablo Franco Martin atakuja na mbinu hii ya 4-2-3-1.

Hii mbinu ni bomba mno Simba SC kwenye kushambulia na kujilinda zaidi kwa viungo wawili wazuiaji "Double Pievort" ambao watakuwa wanaziba space ya fullback akina Kapombe na Hussein wakipanda kwenda kusaidia kushambulia na huku Sakho upande wa kulia na Morrison au Banda upande wa kushoto wakitakiwa "Kuswitch On" muda wote wanapokuwa na mpira na hata wasipokuwa na mpira Incase of Pressing na Movements kushambulia kwa Space pale ASEC Mimosas wanaposhambulia inatakiwa Simba SC kufanya "Turn Overs" ya hatari.

ASEC Mimosas ni wazuri wakiwa na mpira tu ili kuwadhibiti unahitaji kufanya Pressing (kuweka presha muda wote kwenye mpira) huku Midfielders wakifanya majukumu yao ya kuvunja njia za pasi (Cut the passing lane) kwa mbinu hii kufanikiwa ni rahisi kuliko kufeli na hapo upo uwezekano wa kufuzu robo fainali mapema ugenini kwa alama tatu, au kupata alama moja muhimu sana ili kupiga hatua moja kuelekea robo fainali.

Kuna Uwezekano ASEC Mimosas wakavuta pumzi ya moto kutoka kwa Simba SC.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
 
Game itakua open kwa kila timu,timu itakayotumia nafasi vizuri ndio itakayopata matokoe mazuri.
 
Sioni haja ya kwenda kupaki basi Benin, Simba na Asec wote ni wageni leo.
Ila kwa ninamvyomtazamia Pablo mmmh....
Ngoja niwe na akiba ya maneno
Hapa mashambulizi ya kasi na ya hatari pamoja na kujilinda kwa nidhamu ndo suluhisho kama kweli tunahitaji alama ugenini.

Kujilinda muda wote ni sawa na kulamba asali kwa mcha ya kisu.
 
Acheni kujifariji ninyi'' zikipungua sana tatu! Mtarudi kwa aibu
 
Acheni kujifariji ninyi'' zikipungua sana tatu! Mtarudi kwa aibu
ASEC Mimosas watavuta pumzi ya moto kutoka kwa Simba SC

Kwahivyo Mkuu inakuathiri hata wewe..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…