Inawezekana Kujifunza kumpenda mtu?

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
Habari wana jamvi!
Ni kweli kuwa inawezekana kujifunza kumpenda mtu (kimapenzi)
hata kama kwa mara ya kwanza hukumpenda au hakuvutii?
Ufanye nini au ni steps gani za kuzifuata?
 
Habari wana jamvi!
Ni kweli kuwa inawezekana kujifunza kumpenda mtu (kimapenzi)
hata kama kwa mara ya kwanza hukumpenda au hakuvutii?
Ufanye nini au ni steps gani za kuzifuata?

Ndio hilo lawezekana. Kupenda ni kutoa/kujitoa ('giving') na mara nyingi kutoa/kujitoa ni kitu kinachotokana na utashi.

- Jifunze kutoa/kujitoa.
- Weka jitihada kumtambua mtu kwa undani
- Jifunze kutizama na ku appreciate mambo chanya ya mtu na hivyo kujenga mahusiano kwenye mambo chanya.
 
kujifunza kumpenda mtu kimapenzi ni ngumu, lakini ukiishi namtu ambaye humfeel kivile sana, bada ya muda unamzoea sana kiasi ambacho huwezi kumuacha na unaweza kuwa umezoea company yake ile mbaya.......nafikiri ikifika hapo, unakuwa unafanya mambo yote ambayo wapenzi wangefanya au kumfanyia mpenzi, coz u feel real close naye.

hayo nayaita mapenzi ya kuzoeana......inatokea tu, lakini haujifunzi overtime.
 



lakini inasemekana kupenda ni kitu flani 'NATURAL'
So kwa steps hizo hapo juu si utakuwa kama unampigia mbuzi gitaa?
yani utakuwa kama unaulazimisha moyo wako?
 
Inawezekana kabisa.

Labda kizazi cha dot.com kinashangazwa na hili, lakini wazee wetu walikuwa hawapigi misele na mchumba...Mnaonana siku ya siku ya siku na kila mtu anajua hilo!

Hakuna hata mambo ya .."nataka niende nae boutique tukatafute shela la harusi"😡

Siku hizi kwanza mnabanwa na sheria mtoke mkaPIME UKIMWI PAMOJA..HUH!😀

Sasa, inawezekana kabisa mtu ukajifunza taratibu kumpenda mwenzio, hasa kwa jinsi unavyozidi kujua vitu anavyopendelea zaidi!...

Ukiona hapendi ulevi unaweza ukajifunza kuacha chuichui, then unakuta upendo ndani unazidi...muda wa kuwa kwenye stuli mnakuwa pamoja nyumbani mkijadili kiutu uzima haya na yale!

INAWEZEKANA SANA KABISA!
 



Mkuu Paka,
Kwenye kujifunza kuna kufaulu na kufeli.
so inapotokea umefeli na tayari mpo ndani ya ndoa inakuwaje?
Au kwenye swala hili hakuna kufeli?
 
Mkuu Paka,
Kwenye kujifunza kuna kufaulu na kufeli.
so inapotokea umefeli na tayari mpo ndani ya ndoa inakuwaje?
Au kwenye swala hili hakuna kufeli?

Yup ..kufeli kupo ndo maana unaona baadhi ya familia zimezama kwenye lindi la migogoro isiyotatulika!
Jana tulikuwa na sherehe ya UKABILA mtaani. Nikampigia simu jamaa yetu mmoja kumjulisha venue, nikimwagiza waje na mkewe!
Mkuu, jibu nililopata ni hatari..Niliambiwa kuwa nisipompigia mwenyewe huyo mwanamke simu, basi nitegemee kabisa kutomwona!!.Ikabidi nimpandie hewani mwanamke tena once more!
Jamaa alisema hana mawasiliano na mkewe kwa miezi sasa, ni kila mtu anachojua ni kutafuta upande wake kitandani, na kujifunika kivyake!...Nilichoka.
 
lakini inasemekana kupenda ni kitu flani 'NATURAL'
So kwa steps hizo hapo juu si utakuwa kama unampigia mbuzi gitaa?
yani utakuwa kama unaulazimisha moyo wako?

Wenzetu waingereza wana neno 'infatuate' or 'infatuation' ambalo ni tofauti na 'to love' or 'love'. Kama umekusudia infatuation then I think you are right huwezi kujifunza, it will just come!
 
Wenzetu waingereza wana neno 'infatuate' or 'infatuation' ambalo ni tofauti na 'to love' or 'love'. Kama umekusudia infatuation then I think you are right huwezi kujifunza, it will just come!

Mkuu kama hutojali naomba unielezee kinaga ubaga kuhusu hiyo red hapo juu.
 
Kwa mie siamini kama kuna kujifunza kumpenda mtu..
 
Mkuu kama hutojali naomba unielezee kinaga ubaga kuhusu hiyo red hapo juu.

Nadhani hii itasaidia:


 
mapenzi huja autonaturally. yana njia mbili mwa mwanaume (kwa mwanamke sijui); moja ni kwa kuona na kutamani kisha kupenda. ya pili ni kuzoeana na mwanamke na kisha taratibu kuanza kupenda. hii ni tofauti na kujifundisha kupenda. utajifunza mbinu za kufanya mapenzi ila si kupenda
 
Mapenzi yameundwa kwenye mazoea, pasipo na mazoea hakuna mapenzi,
Mapenzi yanakomaa kutokana na mazoea
Mazoea yanatokana na kukaa pamoja au kuwasiliana
Mapenzi pasipo daraja nyongo yatatumbukia
Mapenzi elimu ili daima yadumu
Kujifunza kwawezekana kwenye mapenzi lakini sio kama hesabu
Mapenzi elimu hukifeli dunia utaiona chungu
 
mkuu nakubali kabisa. Hapo kwenye blue panahusika sana, kukaa (sio lazima kukaa chumba kimoja, namaanisha being together) na kuwasiliana vinaendana.
Ukiacha kuwasiliana...mwanangu, mambo yatakuwa sio mambo. yale yale ya story ya PJ
 
Upendo una kawaida ya kupungua na kuongezeka kutegemea na nyie mnajuhudi gani.kwa hiyo inawezekana kujifunza kumpenda mtu.
 
I second that... I think love comes naturally and there is no way u can learn to love someone... for instance there was this guy who really loved me so much, he was a very good guy and treated me very nice but too bad I coudlnt love him back... I tried but coulndt... so I broke up with him

and there was a time I loved another guy I dont even know why I loved him, he use to drive me nut most of the time and we would never stop fighting... but when I was with him I was a totally different person... ...

I'd stopped and think what was wrong with me? why did I have to choose a looser and someone who makes my life so difficult

... sometimes love can be complicated and impossible...
 
Habari wana jamvi!
Ni kweli kuwa inawezekana kujifunza kumpenda mtu (kimapenzi)
hata kama kwa mara ya kwanza hukumpenda au hakuvutii?
Ufanye nini au ni steps gani za kuzifuata?
Swali lako ni pana kuliko unavyofikiria. It needs us to assume a lot of things?Labda ulielezee kiasi...
Mf:
Je, ni mtu ambaye mmezaa naye mkalazimika kuishi pamoja?
Je, ni mtu anayeonekana kukupenda sana kiasi unafeel unfair for not reciprocating his/her love?
Je, ni rafiki yako wa kike/kiume ambaye unaona ana hisia za kimapenzi juu yako na wewe mpaka sasa unamchukulia kama rafiki?
Je, ni mtu ambaye rafikizo wanaona anakufaa na wewe huna hisia naye?
Je...
Tupe the reason behind the question because maswali yote niliyouliza yana majibu tofauti.
Nawasilisha...
 

Kingi nakuelewa. Lakini kama kupenda ni auto'matic' ('naturally'?) kwa nini Mungu aliwaagiza wanaume 'wawapende' wake zao? Katika maagizo haya Mungu alipotumia neno kupenda alikusudia nini?(Sorry, nimetumia biblical angle just to clarify my point).
 


Mkuu ukiacha hiyo 'Je' ya kwanza, lakini 'Je' nyingine zote ndipo swali langu linaangukia hapo.
 
Inawezekana sana kujifunza kumpenda mtu (ila hii wengi husema kwa mwanamke zaidi)

kuna watu huwa mrafiki kwanzoni lakini muda unavokwenda they grow feelings za mapenzi
wengine hutongozwa na watu ambao wala hawawa-feeling lakini muda unavokwenda wakiwasiliana na kuwa na ukaribu hisia za mapenzi huchipua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…