Inawezekana kukopa kwa kutumia hati ya kiwanja.

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
6,016
Reaction score
5,296
Salaam.
Mimi ni mgeni katika mambo ya mikopo sijawai kukopa benki yoyote,nimekua nna nia ya kuchukua mkopo benki nnayo hati ya kiwanja tu,afu kwa sasa sina biashara yoyote as in hiyo hela nikiipata ndo nataka niitumie kama mtaji,naitaji kujua kwa nmb naweza kupata huo mkopo?ama kama kuna benki yoyote naweza kupewa mkopo kwa vigezo vyangu.
Asantrni in advance.
 
Hyo biashara unayotaka kuanzisha kwa mkopo ni gani..... mikopo ni mizuri kama unayobiashara tayari na unataka kuboresha tu
 
Hyo biashara unayotaka kuanzisha kwa mkopo ni gani..... mikopo ni mizuri kama unayobiashara tayari na unataka kuboresha tu

Mkuu kwa hiyo unanishauri niachane na mikopo kwanza,biashara nnayotaka kufanya ni ya used spairs parts za magari.
 
Mkuu kwa hiyo unanishauri niachane na mikopo kwanza,biashara nnayotaka kufanya ni ya used spairs parts za magari.
mkuu hati ya wizara ya ardhi, yaani ya kiwanja kilichopimwa au ni hati ya kimila?
jbu la swali lako ni kweli unaweza kukopeshwa mkopo ukiwa na hati mojawapo hapo juu.

lakini benki hawakopeshi mtu anayeanza biashara wanakopesha mtu mwenye biashara tayari, hii ni kukusaidia wewe binafs biashara unayokwenda kuanzisha bila jua soko litakuwaje kuna ugumu kuliko mtu mwneye biashara tayari mwenye kujua upepo wa soko kabisa ambaye anaweza kufahamu ni kweli kiasi atachokopa ataweza rudisha.
 
Inawezekana mkuu kitaalam inaitwa mortgage,inabid kiwanja kiwe kimepimwa na pia kiendane thamani na mkopo unaouitaji! benki itakachofanya ni kwenda kuisajili kwa msajili wa nyaraka na hati baada ya kuthibitisha hiyo hati,thamani yake na vilivopo kwenye hati na uwepo wa kiwanja hivo mtaandikishana mkataba na utapewa mkopo
 
mkuu hapo unangoma nzito sibora uuze kiwanja uwanze biashara lakini ikatie leseni na tin isajili.itakuwa poa then utakuwa umepata sifa ya mkopo kiulaini lakini hakikisha unakuwa na dhamana ya ziada
 
Hyo biashara unayotaka kuanzisha kwa mkopo ni gani..... mikopo ni mizuri kama unayobiashara tayari na unataka kuboresha tu

ni kweli asikulupuke kuchukua mkopo na kuanza biashara but mikopo ni mizuri uchukue na kuendeleza hatumkatishi tamaa lkn ukweli ni kwamba wengi wameishia kufirisishwa kwa kuchukua mikopo na sasa lyf kwao ni ngumnu
 
Mkuu kwa hiyo unanishauri niachane na mikopo kwanza,biashara nnayotaka kufanya ni ya used spairs parts za magari.
Ingekua vyema kama ungeanza mwenyewe kwanza hata kwa kujibana kisha ukajua ups and downs za hyo business ndio ukaingia kwenye mikopo kwa ajili ya kujiimarisha zaidi...maana biashara ya used spare parts kama huna utaalamu nayo pia inaweza kukugharimu zaidi..ni ushauri tu lakini mkuu,maamuzi bado yanabaki kwako
 
Huwezi kupata mkopo kama huna biashara au hujaajiriwa
Fungua kwanza biashara then ndio ukakope tena uiendeshe kama miezi kadhaa kabla ya kukopa.
 
Mkuu kwa hiyo unanishauri niachane na mikopo kwanza,biashara nnayotaka kufanya ni ya used spairs parts za magari.

Hapo mkuu inatakiwa kuwa makini sana,maana ukichukua mkopo ndo kama mtaji, kuna spare zingine zinachukua muda sana kununuliwa sasa fikiria hapo marejesho yatakuwaje.
 
Labda kama uende CRDB kuchukua mkopo wa KILIMO:

1. Kama una hati ya kimila/hati ya makazi (kwa Dar es salaam) wanakupa hadi mil20
2. Kama una hati ya serikali wanakupa unaoendana na thamani ya kiwanja/shamba

NB: Ukiwa na akaunti hapo CRDB inakuwa rahisi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…