Inawezekana kupata mwenza wa maisha kwenye 40+ jamani

Kijana wa uvccm amepata vijihela vya kwenye kampeni, tayari ameanza kuvurugwa! Yaani ameshasahau kama ndoa inahitaji uvumilivu, uwazi, majadiliano, nk.
Hivi usikute amelipata shangingi la UWT linamuendesha kama gari bovu!
Aisee🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mbona sipo Mimi kwenye timu ya kampeni mkuu
 
Kumbe hata nikiwa mapajani mwa wifi yenu napepewa Bado natoa points namna hii?!!!!
Punguza kutukana watu humu. Uchawa huu wa kihayawani utapita na mianasiasa hii unayoitetea mpaka kujivua utu wako na kudhalilisha wenzio wala haiaminiki. Leo iko hivi na kesho ishakubadilikia. Na karma ipo tu inakusubiri!
 
Nauliza tu Ili nijue kama niachane na huyu mke niliyemuoa miaka 12 iliyopita au nivumilie tu mateso ya kujichubua, dalili za kuchepuka na uvaaji wa madela yanayoonyesha mwili

Ushauri wenu tafadhali.
Yaani miaka 40 bado unawaza kuoa tena mke wa maosha!! Achana na kuwaza ndoa, hapo unakaribiwa na kisukari, presha na magonjwa ya moyo
 
Nauliza tu Ili nijue kama niachane na huyu mke niliyemuoa miaka 12 iliyopita au nivumilie tu mateso ya kujichubua, dalili za kuchepuka na uvaaji wa madela yanayoonyesha mwili

Ushauri wenu tafadhali.

Maisha yako yanatakiwa yakupe furaha mkubwa, kama upo na unateseka age ni namba tu unaweza kuchange dakika yoyote ukaondoa kero, hata kama una miaka 70 acha 40, kwanza bado kijana sana hapo.
 
Hapo dumu 5 nkangala 50 alfu na hela mshenga 5000 unabeba mke live.
Mbuzi,ngombe na taka zote we kubali tu sema zipo home zinamsubiri tu.
Unakopa mnarudi zenu mjini.
Mama watoto wangu alinipa hela ubungo pale nyingi tu nikampe babaake na njiani korogwe kanipa tena na babaake yuko mle.
Tumefika mjini gari likapigwa kona ndani.
Aisee ngombe,kachinjwa tayari,supu,macharali,nyamachoma balaa.
Kikao sasa,nilipiga uongo kanifundisha bibi njia nzima jinsi ya kumdanganya babaake😁,
Nikaona ok,tunafika tu mzee anatoa safari,mkewe sprite,wife anasisitiza gonga safari wewe
Nilipiga tarumbeta nikapewa ingine nikarekebisha tai piga fundo reefu.
ndo nikakaa kumskiliza mangi,
aisee ule uongo Mungu anisamehe tu.
Ila tulimchota akili mzee mpaka akasema karibu nyumbani kwako hapa,aisee sikuamini
Nikapewa na kiwanja na shamba la nguruwe daah.
Nashkuru kijana niko nae sasa miaka 23+.
 
Ilitakiwa niandikeje mkuu? Hebu toa mfano
Ni wewe kweli au kuna mtu amedukua akaunti yako!?
Maana sio kwa huu ustaarabu wa kuandika ambao sijawahi kuuona kwako.

Kuhusu kuoa, unaweza kupata mke wa rika lolote unalotaka, muhimu pesa yako tu.
Ila, jua kwamba wanawake kwa asilimia kubwa wanafanana kwa tabia,ni jukumu lako mwanaume kumbadili ili aendane na mfumo mtakaokubaliiana.

Sasa kama huyo uliye naye mmeishi miaka 12 ni umeshindwa kumshawishi kwa njia yoyote ile ili aishi unavyotaka, basi nakushauri tulizana na huyo kwa maslahi mapana ya watoto wenu(kama mnao).

Kwa hii miaka 40, uwezo wa kuhangaika na tabi za mwanamke mpya ni mdogo..utakuja kuishia pagumu na kufa kwa magonjwa ya moyo.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…