Inawezekana kuuza kiwanja ambacho kiko kwenye process za transfer?

mbenathadeus

New Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
3
Reaction score
0
Habari wanajamii!,tafadhali naomba kujuzwa kama inawezekana kuuza ardhi ambayo nimenunua kwa mtu na nipo kwenye hatua za mwisho za kuaptiwa hati mpya kwa maana nimefanya transfer.nimepata mteja ambaye anataka kununua ardhi hii tena toka kwangu je sheria za ardhi zinaruhusu kumuuzia mteja huyu kabla sijamalizia process za transfer?.
 

Nadhani ni mpaka process ya ku-transfer imalizike na kiwe kwa jina lako. Vipi ulilipa kiasi gani manispaa wakati wa ku transfer? kwani na mimi ninacho kimoja nataka kukitransfer.
 
Yes unaweza kuuza si mali yako bwana, cha msingi tu hati itakapotoka kwa jina lako unayemuuzia atawajibika kufanya transfer ili hati iwe kwa jina lake
 

Sheria hazikuruhusu kuuza mali yoyote ile isiyohamishika ambayo haikuandikishwa kwa jina lako.

Malizia kwanza uhamishaji wa jina kutoka kwa mmiliki wa awali kwenda jina lako. Kimsingi, kufanya kinyume cha hapo ni kukiuka sheria, kwani huna haki ya kuuza kiwanja hicho hata kama umekilipia, kwa kuwa Serikali haitambui umiliki wako.

Acha tamaa.
 

Hapo ni mpaka transfer ifanyike na ikamilike na upate hati yenye jina lako ndio unaweza kuuza, for the time being mmiliki halali ni huyo aliyekuuzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…