Inawezekana kuwachanganya kuku chotara na kuku wa kienyeji?

Inawezekana kuwachanganya kuku chotara na kuku wa kienyeji?

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Habari wadau?

Naomba kuuliza, je, inawezekana kuwafuga kuku chotara na kuku wa kienyeji kwa kuwachanganya katika banda moja?

Yaani, unakuwa na banda moja la kuku hao (kienyeji + chotara) ila unawafuga kienyeji wote kwa kuwafungulia nje ndani ya fensi lakini, na jioni unawafungia ndani (Ufugaji huria).

Binafsi huwa najifunza hapa JamiiForums, nilianza kuuliza banda.

NB: Huku tulipo, kuku wenye soko kwa ajili ya nyama ni wa kienyeji + chotara. Kuku wa kizungu wa nyama bado hawajakubalika au kuzoeleka.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana Mkuu sema uwe unachunguza Mara kwa Mara na kutibu dalili za magonjwa ya kuhara na typhoid hasa kwa hao chotara
 
Back
Top Bottom