Naomba kuuliza, je, inawezekana kuwafuga kuku chotara na kuku wa kienyeji kwa kuwachanganya katika banda moja?
Yaani, unakuwa na banda moja la kuku hao (kienyeji + chotara) ila unawafuga kienyeji wote kwa kuwafungulia nje ndani ya fensi lakini, na jioni unawafungia ndani (Ufugaji huria).
Binafsi huwa najifunza hapa JamiiForums, nilianza kuuliza banda.
NB: Huku tulipo, kuku wenye soko kwa ajili ya nyama ni wa kienyeji + chotara. Kuku wa kizungu wa nyama bado hawajakubalika au kuzoeleka.