Inawezekana kweli kijana kutoka kimaisha katika utawala huu?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
jamani eheee mimi mwenzenu kila nikiangalia vijana wenzangu walionitangulia naona wamerudi nyuma wakati nikifikiria kuhusu plan B katika maisha

nimejaribu kuangalia jamaa zangu waliokuwa wanafanya biashara wengi wanalalamika biashara zimekuwa ngumu, wamefunga biashara zao, nimejaribu kuangalia jamaa zangu walio katika kilimo wanalalamika mambo pembejeo, nimewangalia jamaa zangu ambao wameajiriwa wanalalamika mshahara hautoshi, nimejaribu kuangalia kila kona kila mtu anaongea lake

ivi kweli mambo yenyewe ndo haya ivi kuna kutoka hapa kimaisha kweliiii
 
Nawe endelea kulalamika huku wenzio tunapiga hela katika zama hizi hizi za JPM
 
Jenga nyumba kwenye msingi imara
Usidanganywe na ukubwa mchanga, mvua ikinyesha huwa unaondoka.

Anyways umefanyaje kukubaliana na utafiti kuwa TZ imejintakulia nafasi ya kwanza kwenye medari za uvivu?
 
usikate tamaaaa mkuu panga strategies zako zitekeleze watu wanapiga pesa alafu kama naona jiwe alivyobana watu ndo wanaumiza vichwa kweli
 

Mbona katika Tawala zilizopita hukutuuliza tulifanikiwa nazo vipi ila umeguswa na Tawala hii ya sasa ambayo unaona inatuangusha?
 
Vijana wa CCM .wanatoboa sana Mkuu.Kwa sababu wao sio wapiga madili.Karibu kambini.Kijana wa CCM akianzisha biashara na akatumia ilani ya Uchaguzi ya chama mapema kabisa anatoboa.
 
Kwani mleta mada unatakaje ?
ila nakushauri toka nchini kwanza utarudi 2025
 
Tuombe Mungu avatarmate
 
Mbona katika Tawala zilizopita hukutuuliza tulifanikiwa nazo vipi ila umeguswa na Tawala hii ya sasa ambayo unaona inatuangusha?
hukunielewa mimi nazungumzia issue ya kutoka kimaisha
 
Hakuna Awamu nzuri kama hii. Awamu hii kila mtu anaheshimiwa, wewe fanya kazi halali na kwa bidii uone mambo yako yanvyooka kwa sababu hakuna mtu wa kuja kukuuliza kuwa unamfahamu yeye ni nani !!!
 
Hii awam ina both side mbaya na nzuri.ukitusua unatusua kwelii na ukifulia hadi utoke n shughuli.cha msingi n uvumilivu na kupambana tuu.
 
ni vigumu sana kutoboa kwa hali iliyopo.Yani sasa hivi hata ukijiunga na Freemason au kufanya ndagu ya wakinga bado hutaweza kutoboa
 
Zama hizi si nzuri kwa wapiga mizinga.Maana ukipigwa tu we mtaje magufuli basis umenusurika,mi naamini kuwa kuna watu wanatusua kipindi hiki ila wengi wameamua kuendana na wimbo wa Hali ngumu ili wasiombwe pesa.Ila ukweli ni kwamba watu tumeanza kuwa na adabu na pesa,Nina miezi mingi siijui bia.Ni mwendo wa kahawa na soda/maji.Hiki ni kipindi kizuri cha kumake ili kufungua biashara kubwa hali ikitulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…