Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Naamini bila ya chembe ya wasiwasi kuwa kwa sasa historia ya Iddi Faiz Mafungo inafahamika na wengi.
Iddi Faiz Mafongo Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika aliyesimamia ukusanyaji wa fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955 na mmoja wa watu waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo Agosti 1955, alifariki tarehe 9 Januari, 1987, akiwa na umri wa miaka 75.
Mwaka 1959 alichaguliwa kuwa mweka hazina wa TANU ngazi ya taifa wakati huo huo akiwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Ilikuwa kutokana na uadilifu wake ndiyo alichaguliwa kusimamia hazina ya TANU wakati ambapo uhuru ulipokuwa unakaribia chama kikiwa na fedha nyingi.
Iddi Faiz alikufa mtu masikini na aliyekuwa na kinyongo. Mategemeo yake kwa uhuru alioupigania hayakutimia.
Katika siku zake za mwisho baada ya kustaafu kutoka TANU Press, alikuwa akitumia muda wake mwingi akisoma Qur’an Tukufu.
Alipokufa, Mzalendo gazeti la kila Jumapili la chama alichokiasisi mwenyewe na kukijenga, lilitangaza kifo chake siku mbili baada ya kuzikwa.
Makala ndogo iliyotolewa ilieleza kifo cha mfanyakazi wa zamani na mchango wake katika harakati za kudai uhuru haukugusiwa hata kidogo.
Katika mazishi yake chama hakikupeleka mwakilishi kutoa rambirambi!
Kile kilichompata Abdulwahid Sykes kilimfika Iddi Faiz Mafongo; na kwa bahati wote wawili walikuwa viongozi katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU.
Father James Lynch, muasisi wa St. Francis College alikufa Uingereza siku chache kabla ya Idd Faiz.
Kifo chake kilitangazwa katika gazeti la chama Uhuru (8 January, 1987) na gazeti la serikali, Daily News 8 January, 1987).
Magazeti hayo yakaandika kwa urefu mchango wake katika elimu wakati wa ukoloni.
Iddi Faiz, aliyeasisi TANU, akamuunga mkono Nyerere na kupigania uhuru wa Tanganyika, mauti yalimkuta katika hali ya ufukara nyumbani kwake Magomeni na si chama alichokijenga wala serikali aliyoiweka madarakani ilikuwa na habari ya kifo chake.
Huyu Father Lynch ndiye aliyemuandikia barua Mwalimu Nyerere ya kumtaka achague TANU au ualimu.
Picha: Kwanza kushoto ni Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu.
Picha ya pili aliyesimama kulia kwa Julius Nyerere ni Iddi Faiz Mafongo.