Pre GE2025 Inawezekana watu wasiyojulikana ni kitendawili kwa serikali na polisi lakini ukimya na uzito wao kwenye matukio haya usema vingine!

Pre GE2025 Inawezekana watu wasiyojulikana ni kitendawili kwa serikali na polisi lakini ukimya na uzito wao kwenye matukio haya usema vingine!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Inawezekana matukio haya hasa kwa wapinzani kutekwa na kuuliwa ikawa kitendawili kwa serikali, bado ikawa fumbo kubwa kwao kung'amua nani anahusika na maatukio haya dhalimu, lakini ukimya wao unasema vingine.

Walitakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea na kuchukua hatua haraka pindi tu yanapotokea ama kuripotiwa na wananchi.

Lakini kila wakipelekewa ripoti majibu yamekuwa siyo ya kuridhisha na Spika alipigilia msumari majuzi kuwa matukio haya hayastahili kuangaliwa kwa jicho la tatu na kwa udharura kama wananchi wanavyopata taharuki.

Hitimisho mnalotuachia wananchi ni kuwa ninyi ndio wahusika wakubwa wa matukio haya.

Mkiendelea kukaa kimya wananchi watakuja na mbinu zao ili kupata suluhu.
 
Unajua maana ya KIAPO?
Ukielewa,huwezi kuuliza.
 
Back
Top Bottom