Inawezekanaje? Tanzania yapanda chati kwenye ripoti ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Kama unaishi Tanzania basi bila shaka utakuwa unafahamu kuwa media zetu haziko free kama ambavyo zinatakiwa ziwe.

Suala la kukosoa serikali limekuwa ni nadra sana kusikika kwenye media za Tanzania ambapo media nyingi zimekuwa ni mouthpiece ya chama tawala wakiogopa kuikosoa serikali.

Pamoja na wimbi hilo kutanda nchini Tanzania, ripoti iliyotolewa siku ya jana na Tanzania Centre Of Democracy (TCD) zinaonesha kuwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania umeongezeka.

Soma Pia: Jaji Warioba: Hofu na uoga sababu ya vyombo vya Habari kutoandika matatizo ya Wananchi

Kulingana na ripoti hiyo ni kuwa, kwa sasa Tanzania ni nchi ya 97 kwa kuwa na uhuru mkubwa zaidi wa vyombo vya habari duniani ukilinganisha na mwaka jana ambapo Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya 143.

Swali langu kwenu wanabodi ni kuwa hii inawezekanaje? Au kuna sheria yoyote imebadilishwa wakuu na sisi hatujui? Mbona hali inazidi kuwa mbaya na ripoti inasema tofauti?

Media Chart.png

TCD.png

Nawasilisha!
 
Unashangaa hilo?

@Maxence Mello ana tuzo za uhuru wa habari na nafhani yupo kwenye taadidi ya mambo ya uhuru wa habari Tanzania, wakati huohuo JF tunafichiwa nyuzi, zinabadilishwa majukwaa nyuzi zetu, zinabadilishwa maudhui.

Hakuna uhuru wa habari duniani. Tusijidanganye.
 
Kabisa. Wenye madaraka wanaendesha vyombo watakavyo wao,

Na kimsingi, hakuna njia ya kuwazuia.
 
Wanabodi,

Kama unaishi Tanzania basi bila shaka utakuwa unafahamu kuwa media zetu haziko free kama ambavyo zinatakiwa ziwe.

Suala la kukosoa serikali limekuwa ni nadra sana kusikika kwenye media za Tanzania ambapo media nyingi zimekuwa ni mouthpiece ya chama tawala wakiogopa kuikosoa serikali.

Pamoja na wimbi hilo kutanda nchini Tanzania, ripoti iliyotolewa siku ya jana na Tanzania Centre Of Democracy (TCD) zinaonesha kuwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania umeongezeka.

Soma Pia: Jaji Warioba: Hofu na uoga sababu ya vyombo vya Habari kutoandika matatizo ya Wananchi

Kulingana na ripoti hiyo ni kuwa, kwa sasa Tanzania ni nchi ya 97 kwa kuwa na uhuru mkubwa zaidi wa vyombo vya habari duniani ukilinganisha na mwaka jana ambapo Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya 143.

Swali langu kwenu wanabodi ni kuwa hii inawezekanaje? Au kuna sheria yoyote imebadilishwa wakuu na sisi hatujui? Mbona hali inazidi kuwa mbaya na ripoti inasema tofauti?

Nawasilisha!
Huwa nasikiliza na kuangalia vyombo vya habari vya nje. Jee umefanya hivyo na kufanya tathmini. Tusiojua uandishi wa habari huwa tunadanganywa eti mtu anaweza kuandika chochote, wakati wowote. Hakuna kitu hicho. Kila taaluma ina miiko na taratibu zake.
 
Hiyo ripoti ya CCM imeandaliwa kwenye simple excel sheet isiyoonesha hata x and y axes in fake na ni kutapatapa kwa Samia na CCM yake, hali ni mbaya sasa kama iliyokuwa 2020!
 
Hakuna haki ya habari dunia nzima, msijidai Tanzania tu.

Assange amefanywa nini au kosa lake nini duniani huko?

Evan Gershovick wa Urusi kafanywa nini?

Wanasema hakuna uhuru usiyo na mipaka. Kasoro kwa wakubwa tu wanaoamua mpaka wao ni upi. Kumbuka hilo.

Juzi Mwandishi wa Uingereza nimesahau jna, alikua ana ripoti habariza Assange, katekwa airport Uingereza kawekwa ndani siku kadhaa bila kujuwa kosa lake.

Tusijidanganye wala tusidanganyane.
 
Tatizo la waafrika ni kusubiri wazungu wafanye makosa ili watumie makosa hayo kama miongozo ya kuendesha mambo Afrika. Hili ndilo jambo alilosema Samia akiwa Moshi kuwa hata Marekani shambulio la Trump mbona lilikuwa jambo dogo tu, kwa hiyo anataka na sisi tuchukulie mashambulio na mauaji ya watanzania kuwa jambo dogo tu! Sijui tunapataje viongozi wa aina hii.
 
Huwa nasikiliza na kuangalia vyombo vya habari vya nje. Jee umefanya hivyo na kufanya tathmini. Tusiojua uandishi wa habari huwa tunadanganywa eti mtu anaweza kuandika chochote, wakati wowote. Hakuna kitu hicho. Kila taaluma ina miiko na taratibu zake.
Kama unaangalia vyombo vya habari vya nje bila shaka utakuwa umetokea clips za Fox News, CNN na wengineo zikimwonyesha Rais Biden akianguka jukwaani na kwenye ngazi ya ndege. Aidha, alivyokuwa akiduwaa kwenye mdahalo wake na Trump. Au kukosea majina ya maRais na nchi zao. Clip hizo zikifuatiwa na mjadala kuhusu uzee na utimamu wa akili za Biden kustahili kuongoza Marekani.

Pia utakuwa umetokea kauli za Trump zikikosolewa kwa uongozi na upotoshaji mkubwa. Vilevile habari za Kamala Harris kutokuwa makini na jukumu la kudhibiti mpaka wa Kusini (Mexico border) na mlundikano wa maelfu ya wakimbizi wanaotaka kuingia US.

Kuna media Tanzania inaweza kutangaza na kuandika habari za viongozi wakuu wa serikali za aina hiyo?
 
Tatizo la waafrika ni kusubiri wazungu wafanye makosa ili watumie makosa hayo kama miongozo ya kuendesha mambo Afrika. Hili ndilo jambo alilosema Samia akiwa Moshi kuwa hata Marekani shambulio la Trump mbona lilikuwa jambo dogo tu, kwa hiyo anataka na sisi tuchukulie mashambulio na mauaji ya watanzania kuwa jambo dogo tu! Sijui tunapataje viongozi wa aina hii.
Jitowe basi Umoja wa Mataifa, na mashirika mengine ya Kimataifa. Uliyaanzisha wewe Mwafrika? Au uliomba mwenyewe kujiingiza?
. Unangoja nini?
 
Kama unaangalia vyombo vya habari vya nje bila shaka utakuwa umetokea clips za Fox News, CNN na wengineo zikimwonyesha Rais Biden akianguka jukwaani na kwenye ngazi ya ndege. Aidha, alivyokuwa akiduwaa kwenye mdahalo wake na Trump. Au kukosea majina ya maRais na nchi zao. Clip hizo zikifuatiwa na mjadala kuhusu uzee na utimamu wa akili za Biden kustahili kuongoza Marekani.
Batarajia pia unafuatilia nawe. Unakumbuka ya Rais Mugabe kudondoka na pia mgombea urais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mgombea urais. Hawa wawili wanatoka Afrika, tena Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa hivyo kuripoti ni kwa waandishi wote sio wa Ulaya. Ila kinachoripotiwa kinapaswa kuwa kwa madlahi ya umma.
Pia utakuwa umetokea kauli za Trump zikikosolewa kwa uongozi na upotoshaji mkubwa. Vilevile habari za Kamala Harris kutokuwa makini na jukumu la kudhibiti mpaka wa Kusini (Mexico border) na mlundikano wa maelfu ya wakimbizi wanaotaka kuingia US.
Unazungumzia Trump, rais mstaafu, na Kamala Makamu wa rais wakiwa kwenye kampeni za uchaguzi. Si unajua nini huwa kinasemwa wakati wa ucaguzi? Ulitarajia mtu - mgombea na wafuasi wake - wasifie mpinzani wao?
 
Batarajia pia unafuatilia nawe. Unakumbuka ya Rais Mugabe kudondoka na pia mgombea urais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mgombea urais. Hawa wawili wanatoka Afrika, tena Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa hivyo kuripoti ni kwa waandishi wote sio wa Ulaya. Ila kinachoripotiwa kinapaswa kuwa kwa madlahi ya umma.
Unazungumzia Trump, rais mstaafu, na Kamala Makamu wa rais wakiwa kwenye kampeni za uchaguzi. Si unajua nini huwa kinasemwa wakati wa ucaguzi? Ulitarajia mtu - mgombea na wafuasi wake - wasifie mpinzani wao?
Mipaka ipi ya uandishi unadai lazima ifuatwe katika uhuru wa habari? Leo hii media gani hapa Tanzania inaweza kuandika habari mbaya au isiyomfurahisha makamu wa Rais au Rais mstaafu?

Wakati wa Kikwete kurudi nyuma kulikuwa na uhuru mkubwa zaidi wa habari. Kashfa mbali mbali za serikali zilikuwa kwenye vichwa vya habari vya media. Awamu zilizifuatia, hiyo hali ilipotea kabisa. Ndio maana mleta mada anashangaa Tanzania imewezaje kupanda chati kwenye uhuru wa habari?
 
Mkuu sina hakika kwamba nazungumza na mtu sahihi. Nachelea kusema mambo ambayo yatakuwa kwako ni mageni. Mimi nazungumzia taaluma ya uandishi wa habari na si uandishi. Namaanisha nazungumzia kile kinachoitwa "journalism" na sizungumzii uandishi au kile kinachoitwa "writing". Kwa maana hiyo ni vyema tupumzike tu, nisikuchoshe.
 
Tanzania tuko vizuri, wahuni wachache wakinywa mbege ndio wanakuja kuchafua nchi.
 
Back
Top Bottom