Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Nilipofika kwenye kituo cha mafuta cha maeneo ya Mbezi Beach ya Chini ili kujaza gari langu, niliona mabango mawili yaliyonivuruga kidogo. Moja lilikuwa limeandikwa "Lipa kwa M-Pesa," likinionyesha kwamba naweza kufanya malipo kwa njia ya simu, jambo ambalo niliona ni rahisi na haraka.
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa kulikuwa na bango lingine karibu nalo lililosema "Zima Simu." Nilijiuliza itakuaje nitatumia M-Pesa kufanya malipo wakati nimeambiwa nizime simu yangu?
Nilimwuliza mfanyakazi wa kituo cha mafuta kuhusu hali hiyo, naye kabaki anacheka tu.
Hii imekaaje wadau?