Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
TUMEGUSWA mno na habari zilizotoka katika vyombo vingi vya habari juzi kwamba, hatimaye Serikali imekiri kuwa, udanganyifu unaofanywa na wanafunzi katika mitihani ya kitaifa ni mkubwa na kusema ni janga la taifa linalohitaji hatua za haraka kuudhibiti hasa katika shule za Serikali.
Katika kuonyesha ukubwa wa tatizo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo aliliambia Bunge juzi kwamba wizara yake imegundua kwamba shule za Serikali ndizo zilizoongoza katika uchakachuaji wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi iliyofanyika mwaka jana na kusema kuwa, wakati shule za binafsi zilizogundulika kufanya udanganyifu zilikuwa 32, shule za Serikali zilizofanya hivyo zilikuwa 300.
Akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola aliyedai Serikali haikuwatendea haki wanafunzi 9,736 waliofutiwa mitihani yao na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), 361 kati yao wakiwa katika Wilaya ya Mufindi ambapo sasa watatakiwa kurudia mitihani hiyo Septemba mwaka huu, Mulugo alisema msimamo wa Serikali hauwezi kubadilika na kwamba adhabu iliyotolewa ni kwa mujibu wa sheria za nchi.
Msimamo huo wa Serikali unakuja wakati zipo taarifa za kushtusha kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajui kusoma wala kuandika na kwamba Serikali inapanga siyo tu kuwaachisha masomo, bali pia inaangalia uwezekano wa kuwachukulia hatua za kisheria wanafunzi hao na wakuu wa shule wanazotoka. Idadi hiyo ya wanafunzi ni ya mikoa yote ya Tanzania Bara, isipokuwa Kigoma ambao taarifa zake hazijawasilishwa wizarani. Kwa maana hiyo, ni wazi kwamba takwimu za mkoa huo zikiwasilishwa wizarani idadi ya walioingia sekondari bila kuwa na sifa bila shaka itaongezeka.
Idadi hii ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika, licha ya ‘kufaulu' mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuchaguliwa kuingia kidato cha tano mwaka huu ni kubwa mno kwa kigezo chochote kile. Hiki ni kitendawili kinachopaswa kuteguliwa haraka iwezekanavyo na tunayo kila sababu ya kuelekeza lawama kwa vyombo vya usalama kwa kushindwa kugundua mtandao huo wa kuchakachua mitihani hadi kuachwa ukaenea nchi nzima bila kugundulika. Ndiyo maana tunakubaliana na Waziri Mulugo anaposema kwamba uchakachuaji huu sasa ni janga la taifa.
Ni janga la taifa kwa sababu uchakachuaji wa mitihani sasa unaonekana kujipa mfumo wa kitaasisi. Kwamba mwanafunzi anaweza kumaliza elimu ya msingi bila kujua kuhesabu, kusoma wala kuandika na akaingia sekondari hadi kidato cha nne hakika haiingii akilini. Ni kwa bahati nasibu tu kwamba wanafunzi hao 5,200 wamegundulika kutojua kusoma na kuandika baada ya kupewa majaribio ya kupima uwezo wao baada ya kuripoti shuleni kama ilivyoagizwa na Waziri Mulugo mwenyewe.
Itakumbukwa kwamba alipotangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba Desemba mwaka jana, Mulugo aliagiza kwamba wanafunzi wote ambao wangeingia kidato cha kwanza mwaka huu, kwanza wapimwe uwezo wao wa kusoma na kuandika. Agizo hilo lilitokana na udanganyifu uliojitokeza katika mtihani huo, ambao kama tulivyosema hapo juu, wanafunzi 9,736 walifutiwa matokeo kati ya wanafunzi 9,83,545 waliofanya mtihani huo.
Hilo hakika ndilo janga la kitaifa. Tunapojenga mifumo ya kitapeli ya kuzalisha wataalamu ‘vihiyo' matokeo yake ni makandarasi wanaojenga madaraja, majengo na barabara mbovu zilizo chini ya viwango; madaktari wanaopasua wagonjwa vichwa badala ya kufanya operesheni za miguu; au matapeli na vihiyo wengine waliomo katika ajira nyeti katika sekta za kilimo, elimu, viwanda, usafirishaji, nishati, maji, uchumi na nyinginezo.
Janga hilo ndilo limetufikisha hapa tulipo, miaka 50 ya Uhuru bado tunaogelea katika umaskini wa kutisha licha ya rasilimali lukuki zinazotuzunguka. Katika hili, haitoshi kwa Waziri Mulugo kugundua tatizo na kukubali tu kwamba ni janga la taifa. Kinachohitajiwa sasa siyo maneno, bali ni dawa ya kukomesha janga hilo la udanganyifu katika mitihani.
Chanzo: Inawezekanaje wanafunzi 5,000 waliofaulu wasijue kusoma, kuandika?