Kwanza huu uzi hapa nilipo uweka ndiyo pake au nimekosea?Maana naona jukwaa la Lugha upo,Elimu upo na hata jukwaa la siasa upo.Kila siku nasikia waliofaulu kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika,Hivi ni waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza au walioteuliwa kujiunga na kidato cha kwanza? na kama wamefaulu au wameteuliwa kujinga na elimu ya sekondari ni vigezo gani vilivyo tumika? na hao ambao hawakufaulu/kuteuliwa wako katika hali gani?JF naomba tulijadili ili tujue elimu yetu ya bongo.