Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Tarehe 04 July kwa Wamarekani ni siku ya kusheherekea uhuru wa nchi hiyo na siku hii ni ya mapumziko. Miaka 240 iliyopita 1776 tarehe 4 July Congress ilitangaza Uhuru wa makoloni 13 ya Marekani na pia yalijitangaza kuwa ni taifa moja la United States of America na hawakuwa tena chini ya himaya ya Kifalme ya Uingereza. Siku hii huwa inashangiliwa na miali ya moto (fireworks) gwaride, nyama ya kuchoma, mchezo wa baseball, familia kukutana, hotuba za viongozi, sherehe, na ni Siku ya Kitaifa.
Watu wa matabaka na rangi zote walivyosherehekea uhuru wa Marekani 04 July, 1776
Uhuru wa Marekani, kisheria uliotoa makoloni 13 kutoka kwenye utawala wa Uingereza ulitokea tarehe 2 July, wakati baraza la wawakilishi wa Makoloni 13 lilipokutana na kupigia kura uhuru ambao ulipendekezwa na Richard Henry Lee kutoka Virginia na kutangaza Marekani iko huru kutoka katika utawala wa Uingereza. Baada ya kura hiyo, baraza lilisubiri kutangazwa kwa uhuru, kucheleshwa huko kwa kutangazwa kulielezewa kama mataarisho ya Mkutano wa watu watano akiwemo Thomas Jefferson kama mwandishi mkuu. Congress ilileta mjadala na kurudia tena neno hadi neno kuhusu tangazo la uhuru, hatima ya mwisho ilifikiwa siku mbili baadae tarehe 04 July, siku moja kabla ya hapo, John Adams alimwandikia mke wake Abigail:
"Tarehe 2 July 1776 itakuwa siku ya kukumbukwa kuliko siku nyingine zote katika hisotria ya Marekani. Ninauhakika siku hii itasherehekewa na vizazi hata vizazi kwa shere kubwa. Ningependea ikumbuke kama siku ya mapokeo kwa mapenzi na moyo wote kutoka kwa Mungu Mwenyezi. Ningependa watu wafurahie kwa shangwe, michezo, kengele, na bonfire kutoka sehemu moja ya nchi mpaka nyingine leo na hata siku zijazo".
Maono ya Adam yalichelewa kwa siku mbili zaidi, matokeo yake Wamarekani walifurahia uhuru tarehe 4 July, ni siku ambayo imetangazwa na inafahamika kuwa ndiyo siku ya Uhuru kuliko tarehe 2 July, siku ambayo mikakati ya uhuru ilikamilika na mjadala kufungwa na Congress.
Wanahistoria walibishana sana kuhusu wajumbe wa Congress kusaini na kutangaza siku ya uhuru kuwa 4 July, ingawa Thomas Jefferson, John Adams na Benjamin Franklin wote baadae waliandika kuwa walisaini mkataba huo siku hiyo. Wanahisoria wengi wamehitimisha kuwa Azimio lilisainiwa tarehe 2 August 1776 na sio tarehe 4 July siku ambayo wote wanaamini.
Tukio la ajabu ni kuwa wote John Adams na Thomas Jefferson, ambao ndio watia saini pekee kwenye Azimio la Uhuru baadae walikuja kuwa marais wa Marekani, walikufa siku moja tarehe 4 July 1826, ikiwa ni miaka 50 ya Uhuru. Ingawa hakusaini Azimio la Uhuru, James Monore ambae ni baba mwingine wa kupigania uhuru ambae alichaguliwa kuwa rais pia alikufa 4 July 1831, alikuwa rais wa tatu mfululizo kura siku ya maadhimisho ya uhuru. Calvin Coolidge, ambae ni rais wa 30 alizaliwa 4 July 1872; yeye ndiye rais pekee wa marekani mpaka sasa hivi ambae alizaliwa siku ya uhuru.
Matukio ya Muhimu:

- Katika mwaka 1777 mizinga 13 ilirushwa na heshima (salute) asubuhi na jioni, 4 July katika Bristol na Rhode Island. Philadelphia walisherehekiea mwaka wa kwanza wa uhuru kwa mtindo ambao mpaka leo unatumika: dhifa ya kitaifa kwa Congress, mizinga 13 na salute, hotuba za viongozi, sala, mziki, gwaride. Meli zilipakwa rangi nyeupe, blue na nyekundu.
- Mwaka 1778, kutoka makao yake makuu Ross Hall karibu na New Brunswick, New Jersey, Generali George Washngton aliazimisha 4 July na vipimo viwili vya ram kwa askari na salute kutoka kikosi cha silaha. Upande mwingine wa bahari ya Atlantic mabalozi John Adams na Benjamin Franklin walihodhi chakula cha jioni kwa Wamarekani wenzao Paris, Ufaransa.
- Mwaka 1779, 4 July iliangukia Jumapili. Hivyo sherehe zilifanyika tarehe 5 July.
- Mwaka 1781 Mahakama ya Massachusetts ilikuwa ya kwanza kuidhinisha 4 July kama siku ya kitaifa.