BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mshindi wa bahati nasibu ya India amesema anaelemewa sana na maombi ya misaada ya kifedha kiasi kwamba anajuta kushinda Bahati Nasibu hiyo.
Anoop, dereva wa magari kutoka jimbo la kusini la Kerala, alishinda rupia 250m ($3.06m, £2.9m) katika bahati nasibu ya serikali mapema mwezi Septemba. Lakini wiki moja baadaye, alichapisha video akiomba watu asiowajua waache kumsumbua yeye na familia yake.
Anoop anasema kwenye video hiyo kwamba anafikiria kuhamisha makazi yake ili kuepuka usumbufu mwingi wa umma. Alinunua tiketi tarehe 18 Septemba - siku moja kabla ya kwenda hadi Malaysia kwa ajili ya kazi.
"Nilifurahi sana niliposhinda," anasema kwenye video yake ya hivi majuzi. "Kulikuwa na watu na kamera nyumbani na tulifurahi."
Lakini hivi karibuni hali imetokea na nashindwa kuidhibiti, anasema.
"Siwezi kutoka nyumbani, siwezi kwenda popote. Mtoto wangu ni mgonjwa na siwezi kumpeleka kwa daktari."
Anoop ambaye atapokea Tsh. Bilioni 4.2 baada ya ushuru wa serikali anasema watu wanaanza kuwasili nyumbani kwake kila asubuhi. "Ninachoweza kumwambia kila mtu ni kwamba bado sijapata pesa. Hakuna anayeonekana kuelewa shida yangu, haijalishi ninasema mara ngapi," anasema.