Che Kadewele
New Member
- Nov 7, 2022
- 2
- 1
Habarini wakuu, naomba kuelimishwa juu ya mada tajwa hapo juu. Tumezoea mara nyingi Watanzania wakikosa huduma fulani kwenye hospitali zetu za ndani basi kimbilio lao ni India, hii inamaanisha katika mataifa yote duniani India imekuwa namba moja kwenye masuala ya afya au vipato vya Watanzania wengi havimudu gharama za hospitali za mataifa mengine ambayo ni bora kuliko India?
Imekuwa kama desturi ya taifa sasa, maana hata ukitazama maigizo yetu ya sinema (bongo movies) mgonjwa akishindikana kutibiwa basi madaktari huwa wanashauri mgonjwa apelekwe India. Hata huku mtaani mjadala mkuu wa maswala ya afya basi hitimisho huwa ni India na sio taifa lingine.
Naomba nielimishwe juu ya hili, vipi hii tabia ya kukimbilia India kimatibabu ni ya Watanzania tu au India ni kimbilio la mataifa mengine ya kiafrika, Ulaya na American?
Natanguliza shukurani.