Tetesi: India: Mama wa kambo 'aamrisha' mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 9 kubakwa na genge

Tetesi: India: Mama wa kambo 'aamrisha' mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 9 kubakwa na genge

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Maafisa wa polisi wamewakamata watu sita kuhusiana na ubakaji wa kikundi na mauaji ya msichana wa miaka tisa nchini India katika jimbo la Kashmir.
_99155146_gettyimages-451906075.jpg

Maafisa wanasema kuwa mama wa kambo wa msichana huyo alimwambia mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 14 na wengine watatu kumbaka msichana huyo mbele yake.

Wanasema kuwa mwili wa msichana huyo ulipatikana siku ya Jumapili katika msitu wilayani Baramulla.

Aliteswa na mwili wake kuchomwa na tindi kali , waliongezea.

Mama huyo wa kambo anadaiwa kukasirishwa kwa kuwa msichana huyo alikua akipendwa sana na mumewe.

Maafisa wa polisi waliambia BBC Urdu kwamba msichana huyo alitoweka kwa siku kumi kabla ya mwili wake kupatikana.


Ilibainika kwamba mama huyo wa kambo alikuwa na chuki dhidi ya mke wa pili wa mumewe na watoto wake , mtandao wa kituo cha habari cha NDTV kilimnukuu afisa mmoja wa polisi Miir Imtiyaz Hussain akisema.

Bwana Hussein alisema kuwa msichana huyo aliuawa kwa shoka baada ya kubakwa na genge.
 
Dah! Hapa ndipo ile kauli ya mama wa kambo inapotumika kuiharibu jamii nzima.

Pole yake mtoto
 
Back
Top Bottom