Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 337
- 296
I
Na Mwandishi Maalum
Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan amesema, Waziri wa Elimu nchini India amemualika Waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania Prof. Adolf Mkenda kuzuru nchini humo ili kujifunza zaidi mambo yahusuyo Teknolojia pamoja na uhandisi kwa lengo la kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Balozi Pradhan, alitoa kauli hiyo juzi Julai 5/2022, alipomtembelea Waziri Profesa Mkenda ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha mahusiano zaidi kupitia Nyanja ya elimu,sayansi na Teknolojia.
Alisema serikali ya India ingependa kwa haraka iwezekanavyo kuanzia mwakani kuona wanafunzi wa kada mbali mbali wanadahiliwa kwa ajili ya masomo yanayohusu teknolojia.
Kwa Upande wake Prof Mkenda, alimueleza balozi Pradhan kuwa serikali,amepokea mwaliko huo wa kutembelea nchini India kwa ajili ya kujifunza na kutengeneza mazingira mazuri ya kuifanya nchi ya India kuanzisha Taasisi ya Kiteknolojia ya India nchini Tanzania itakayofundisha mambo ya Uhandisi pamoja na Teknolojia ya Mawasiliano.
Waziri Mkenda alisema kuwa Balozi huyo amekwisha kutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kumueleza kusudio hilo hivyo Wizara ya Elimu itatafuta eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Taasisi hiyo.
Pia amesema kuwa baada ya kutembelea nchini India atamualika Waziri wa Elimu wa India kuzuru nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea maeneo ambayo yatakuwa yameainishwa kwa ajili ya ujenzi ili kuwa na makubaliano ya haraka ya ujenzi.
Amesema kuwa eneo pekee ambalo Wizara imelifikiria kwa haraka ni Chuo cha Ufundi Dodoma ambacho kitakamilika Disemba mwaka huu na kuanza udahili wa wanafunzi 1500 vilevile chuo cha Tehama ambacho Rais Samia ameagiza kijengwe Jijini Dodoma.
Kadhalika, Waziri Mkenda amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ingependa kuongeza mahusiano kwenye vyuo vya Ufundi ikiwemo VETA kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi.View attachment 0R1A1785.JPGView attachment 0R1A1802.JPG