radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,440
- 32,260
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage amepokea malalamiko kutoka India kuhusu utapeli uliofanywa na madalali wa mazao kutoka Tanzania.
Hivyo taarifa kutoka India zinamtaka kwenda nchini huko kusafisha jina la Tanzania baada ya madalali hao kulichafua kwa kufanya utapeli.
“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira ilisababishwa uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.
Akifafanua zaidi, Mwijage ameeleza kuwa matapeli hao walifanya utapeli kwa kuwadanganya wafanyabiashara huko India kuwa wanapoagiza mazao wanapaswa kutoa pesa ya kianzio dola za Kimarekani 123,000 ambayo ni sawa na shilingi Mil.275 za kitanzania na dola 200,000 ambayo ni sawa na Sh.448 mil za kitanzania.