India yailalamikia Tanzania kwa utapeli, Mwijage kushughulikia suala hilo

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage amepokea malalamiko kutoka India kuhusu utapeli uliofanywa na madalali wa mazao kutoka Tanzania.

Hivyo taarifa kutoka India zinamtaka kwenda nchini huko kusafisha jina la Tanzania baada ya madalali hao kulichafua kwa kufanya utapeli.

“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira ilisababishwa uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.

Akifafanua zaidi, Mwijage ameeleza kuwa matapeli hao walifanya utapeli kwa kuwadanganya wafanyabiashara huko India kuwa wanapoagiza mazao wanapaswa kutoa pesa ya kianzio dola za Kimarekani 123,000 ambayo ni sawa na shilingi Mil.275 za kitanzania na dola 200,000 ambayo ni sawa na Sh.448 mil za kitanzania.
 
Hao wahindi siwapendi kinoma ni wanyonyaji sana kwnye makampuni yao hapa nchini kutapeliwa ni halali yao
Unataka kila siku tutapeliwe sisi tuuu!!!
 
Waache wapigwe wajinga hao;kwanza kuna Baja gani ya yeye kwenda kuwabembeleza?.Kuna watanzania kibao wanatapeliwa huko nje mbona hata siku moja hatujawai kuwatetea.Hao ni wapuuzi wanataka kutumia excuse hiyo ili kuwanyonya wakulima kwa bei zao za kilofa.Leo mbaazi inanunuliwa kwa Tsh 300,mbona hajaja mikoa ya kusini kujieleza?yeye anataka kupanda ndege tu!Ndugu zangu tuna safari ndefu sana .
 
Soko la india si la kubeza,waziri aende haraka sana.

Wahindi idadi yao ni kubwa sana wako bilioni na milioni mia tatu
 
Juzi kuna Thread ilisema mwijage katumwa India, kwenda kuweka mambo sawa mbona Jana alikuwa pale kwenye ripoti ya tanzanite na almasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…