INDIA YAWAPA MEDALI MASHUJAA WA MADOLA
Na John Mapepele
Serikali ya India imewapongeza mashujaa wa Tanzania waliorejea na medali kutoka kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyomalizika hivi karibuni nchini Uingereza.
Zawadi na Medali hizo zimetolewa na Ubalozi wa India kwa wachezaji watatu (Felix Simbu, Kassim Mbundwike na Yusufu Changalawe) leo Agosti 15, 2022 kwenye hafla maalum ya kusherekea siku ya Uhuru wa India kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amekuwa Mgeni wa heshima.
Kiongozi Mkuu wa timu ya Tanzania kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ameshukuru Serikali ya India kwa kuwapongeza na kuwapatia medali washindi wa mashindano hayo.
Amefafanua kuwa Tanzania imeandika historia ya kurejea na medali baada ya miaka 18 ya kutorudi na medali yoyote kwenye mashindano haya.
Aidha, amesema mafanikio haya yamepatikana kutokana na mchango mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anaoutoa kwenye michezo.
Amefafanua kuwa kwa mara ya kwanza katika kipoindi hiki Serikali ya Rais Samia ilighariamia timu hiyo kuanzia Januari tofauti na miaka mingine ambapo hugharimiwa katika kipindi kifupi.
Ametumia nafasi hiyo pia kuushukuru ubalozi wa India nchini kwa kutoa kocha wa mchezo wa Kabadi ambaye ataifundisha timu ya Taifa iliyofuzu kwenye mashindano ya dunia.
Pia ameipongeza India kwa kushika nafasi ya nne kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola.