TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Serikali inapambana kuwahamisha wa Maasai Ngorongoro pasipo sababu za msingi pasipo kuangalia athari kuu, wamaasai na wa Handzabe si sawa na wana kizimkazi ni watu watofauti Kabisaaa.
Hili suala la wa Maasai litaitia Tanzania katika matatizo makubwa kimataifa. Kama wenye mamlaka hawajui, napenda niwaeleze kuwa wa Maasai kwa mujibu wa sheria za kimataifa, si sawa na wa Tanzania wengine. Si sawa na sisi waPangwa, au waJita, au waSukuma. WaMaasai wako katika jumuia ziitwazo “indigenous peoples.”
Tunalo tangazo la kimataifa la haki za binadamu. Hili linafahamika, na linatuhusu wote. Lakini kuna pia tangazo la kimataifa linalowahusu hao “indigenous peoples” pekee, ambalo linaitwa “The United Nations Declaration on the Rights of Indigenous Peoples.”
Kama serikali ya CCM hailijui tangazo hilo, basi ifanye hima kulisoma.
Tangazo hili linasema wazi kuwa “indigenous peoples” wasihamishwe kutoka kwenye maeneo yao, bila hiari au uamuzi wao, na bila wao kufahamu kinaganaga suala zima.
Soma Pia: Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673
Tangazo linasema kuwa watu hao wanayo haki ya kuishi katika maeneo yao, kufuata mila na desturi zao katika maeneo yanayoendana na ibada zao za jadi, kuwafundisha watoto wao mila hizo.
Hata kuhusu hiki kinachoitwa maendeleo, tangazo linasema kuwa “indigenous peoples” ndio wenye haki ya kuamua wanataka nini kimaendeleo. Hizi hoja tunazozisikia hapa Tanzania, kuwa eti tumewajengea nyumba, tumewawekea umeme kule tulikowahamishia, hazikubaliki kama utetezi wa kuwahamisha “indigenous peoples.”
Na kadhalika. Ni wazi kuwa serikali ya CCM imekiuka hayo, na imejiweka katika hali ya kuchukuliwa hatua hasi kimataifa.
Kwa maana hiyo, ni wajibu wa kila mzalendo kupinga hayo yanayofanywa na serikali ya CCM dhidi ya waMaasai. Kupinga huko ni wajibu wa kila anayeheshimu haki za binadamu, na ni wajibu wa kizalendo. Tuinusuru nchi yetu dhidi ya janga linalotunyemelea.
Kama serikali ya CCM ina hoja kupinga hoja hizi, ije itoe hoja tusikilize. Tunahitaji malumbano ya hoja, si mabavu na vitisho kama inavyofanywa na mamlaka.