Robidinyo
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 4,043
- 8,686
Herry Wirawan (katikati) mkuu wa shule ya wasichana ya Kiislamu aliyepatikana na hatia ya kubaka wanafunzi, akisindikizwa na maafisa wa usalama wakati wa kusikilizwa kwa hukumu katika mahakama ya wilaya ya Bandung, Java Magharibi, Indonesia, Februari 15, 2022. Rafi Fadh / AP
Mahakama moja ya Indonesia siku ya Jumanne ilimuhukumu mwalimu wa somo la dini ya Kiislamu kifungo cha maisha jela kwa kuwabaka wanafunzi 13 wa kike.
Wanane kati yao walio na umri wa kati ya miaka 12 hadi 16 ni wajawazito kulingana na uchunguzi wa polisi.
Kesi hiyo inaangazia unyanyasaji katika baadhi ya shule za mabweni ambazo nyingi ni vituo vya mafunzo ya kiislamu.
Jaji aliamuru kwamba mwalimu Herry Wirawan, aliwanyanyasa kingono wanafunzi hao na kwamba baadhi yao walijeruhiwa vibaya.
Tabia ya Wirawan iligunduliwa mnamo mwezi Mei mwaka uliopita wakati mzazi wa msichana mmoja alipotangaza kwamba mwanawe wa kike ni mjamzito.
Viongozi wa mashtaka walimtaka mwalimu huyo kuhukumiwa kifo ama hata kuchinjwa kwasababu uhalifu alioutenda ulikuwa mbaya na ulifanyika kati ya mwaka 2016 hadi 2021.
Serikali ya Jakarta imetangaza kwamba itawalipa karibia dola 6000 kama fidia kila msichana aliyeathirika.