GE2025 INEC yatoa Uamuzi wa Rufaa 38, kwa Ubunge zimekubaliwa nne na saba zimekataliwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 53 na 65 vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 vikisomwa pamoja na kanuni ya 29(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea jumla ya rufaa hamsini na moja (51) za kupinga uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kuhusu pingamizi za Uteuzi wa wagombea Ubunge katika Jamhuri ya Muungano na Udiwani kwa Tanzania Bara.


Kati ya rufaa hamsini na moja (51) zilizopokelewa na kufanyiwa uamuzi, rufaa ishirini (20) ni za kupinga uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kuhusu Ubunge na rufaa thelathini na moja (31) ni kupinga uamuzi kuhusu Udiwani.

Aidha, rufaa kumi na tatu (13) kati ya rufaa hamsini na moja (51) zilitolewa uamuzi katika kikao cha Tume cha tarehe 31 Agosti, 2025 na taarifa yake ilitolewa kwa Umma tarehe hiyo.

Tume katika kikao chake kilichofanyika kuanzia tarehe 01 hadi 03 Septemba, 2025, imefanya uamuzi wa rufaa thelathini na nane (38), ambapo kwa rufaa za Ubunge, Tume imezikubalia rufaa nne (04), imekataa rufaa saba (07) na kufuta…

 

Attachments

Hao ACT wameanza kunyolewa kabla ya uchaguzi. Taratibu tu tutaongea lugha moja. Samia atashinda kwa 99.9% huu uchaguzi na wabunge wa CCM watakua 100% ya bunge!! sijui Act watasema nini tena waaminike. If anything uchaguzi huu utaiongezea Chadema umaarufu!! Na kufuta credibility ya vyama vingine vya upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…