Infidelity ingekwisha kwa wazo hili?

HorsePower

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Posts
3,612
Reaction score
2,567
Sielewi kwa nini wazo hili limenijia kichwani ghafla sasa hivi, ila ngoja niwashirikishe!

Nafikiria kama ningekuwa na uwezo wa kufanya mabadiliko ya system ya utendaji kazi wa akili, utu, upendo, huruma, fahamu na viungo vya binadamu vinavyompa raha, ningefanya mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa mahusiano kwenye ubongo wa mwanadamu, hasa Hypothalamus na limbic system achilia mbali hiyo 'medulla oblongata' yake! Ningeweka formula kuwa kila mwanamume au mwanamke ambaye ameingia kwenye ndoa, basi utashi au ile hali ya kupenda mtu yeyote asiye mpenziwe isifanye kazi. Na pia kama atajilazimisha basi viungo husika vinagoma kufanya kazi. Kamani mkaka basi ile asili yake inakwenda alijojo (inakuwa disabled), na kama ni mdada basi ile kitu inakuwa haifunguki kabisa isipokuwa kwa mpenziwe mmoja tu!

Nahisi hii ingekuwa suluhu ya matatizo lukuki ya ndoa yanayoibuliwa kila siku hapa jamvini, na infidelity ambayo inaelekea kuhalalishwa. Nawaonea huruma waliokumbwa na mikasa kama hii, ambao kiukweli nisingependa waendelee kupata maumivu ya kutendwa ili wawe na muda muafaka wa kuifurahia dunia huku wakimshukuru Mungu aliyeiumba, badala ya kuilaani na kijalaani kwa kuletwa duniani. kama hili lingewezekana, inf ... ingefanikiwaje? Watu wangeishi kwa raha sana!
Ni mtizamo tu ....!

Sijui wenzangu mnauonaje mtazamo huu?

Wenu,

HP
 
Infidelity is part of human nature. Human nature can't be abandoned. Therefore, infidelity is there to stay no matter how deep in denial some might be. That's just the cold hard truth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…