Inflation imeshuka kutoka 19.5% hadi 10%

Nyamuleha jr

Senior Member
Joined
Feb 20, 2013
Posts
185
Reaction score
65
Nimafanikio makubwa kupunguza 9% ya mfumuko wa bei hayo yalisemwa bungeni kipindi cha mkapa inflation ilikuwa 5%
 
Imeshuka wapi? Tanzania hii? Inflation maana yake ni mfumuko wa bei ya bidhaa zinazotumiwa nara kwa mara yaani "consumer products" Sasa bei za bidhaa hizi ilishuka lini?

Hii itareflect kwa wakubwa pekee .......... ila sie wapanda daladala, waendao gengeni bado tupo na inflation yetu ya takribani 30% wala sio 19.5%
 
Imeshuka wapi? Tanzania hii? Inflation maana yake ni mfumuko wa bei ya bidhaa zinazotumiwa nara kwa mara yaani "consumer products" Sasa bei za bidhaa hizi ilishuka lini?

Nami nashangaa ........ kumbe sasa hv tumeanza kwenda mwendo wa data za uongo baada ya wapinzani kuonekana kuwa wanatumia data zinazotolewa na taasisi za kiserikali kuwasulubu serikali na data zao!!!!
 
Hueleweki!
Tulia uwasilishe thread ambayo inaweza kujadiliwa!

Kasikia tu na kuanza kufurahia.....mwache afurahi kidogo apate matumaini angalau ya muda kidogo, kabla hajaenda kuweka gari mafuta km ana gari....then aje aandike tena kuhusu infalation
 
Bongo unapataje a standard basket of goods and reliable indexes given the lack of a coherent system?

Kwa nini nisione hizi figures kama theoretical zaidi?

Inflation figures hizi zinapatikanaje? Na uhakiki kwamba zina uhusiano na ukweli wa mambo unafanywaje?
 
Imeshuka wapi? Tanzania hii? Inflation maana yake ni mfumuko wa bei ya bidhaa zinazotumiwa nara kwa mara yaani "consumer products" Sasa bei za bidhaa hizi ilishuka lini?

kilichoshuka siyo bei bali kiwango cha upandaji wa bei. Mfano bei ya mchele april 2012 tsh 1000, iwapo inflation rate ni 19.5 maana yake bei april 2013 ni tsh1195. Inflation rate ikiwa 10% ina maana bei tsh 1100 april 2013.
 
Hii itareflect kwa wakubwa pekee .......... ila sie wapanda daladala, waendao gengeni bado tupo na inflation yetu ya takribani 30% wala sio 19.5%

sasa wewe ulifikiria inflation itareflect kwa masikini?hizo ni data zao hao mafisani wanajitengenezea wenyewe kwa ajili ya reference zao na sio wewe
 
Imeshuka wapi? Tanzania hii? Inflation maana yake ni mfumuko wa bei ya bidhaa zinazotumiwa nara kwa mara yaani "consumer products" Sasa bei za bidhaa hizi ilishuka lini?

Eneo hili halina wachambuzi kabisa katika vyombo vya habari. Mi naamini hali iliyopo katika uchumi wetu wangekuwapo wachambuzi kwenye vyombo vya habari tungesikia maneno kama Deep Recession, au hata aina fulani ya Depression. Wao wanasimulia tu habari za Dr. Slaa na Dr. Kikwete na michapo ya kina Jack Zoka. Zile ishu za alisema, alisihi, amewataka. CPI wataijulia wapi.... Wakiona figures wanaona maluelue
 
Sasa hizo bei kwenu zimeshuka? Kwetu bado kiwango cha bei ni kile kile hakijashuka so inflation bado iko pale pale au inazidi kupanda tu. Hata bei ya dollar inaashiria kupanda kwa inflation maana nadhani ni zaidi ya 1600.
kilichoshuka siyo bei bali kiwango cha upandaji wa bei. Mfano bei ya mchele april 2012 tsh 1000, iwapo inflation rate ni 19.5 maana yake bei april 2013 ni tsh1195. Inflation rate ikiwa 10% ina maana bei tsh 1100 april 2013.
 
Nimewahi kuuliza, je nitapata wapi tovuti au Tv au radio ambayo inachambua masuala ya uchumi wa Tanzania? Sikuwahi kupata jibu.
Kwa uelewa wangu mdogo, mtu anaposema 'inflation' inapaswa aseme baya kama ni consumer price index, producer price index au GDP deflator. Pia masuala ya riba, uwekezaji, mikopo, uchambuzi wa sera ya fedha, sera ya matumizi ya umma (fiscal policy) n.k.
Kama aliyosema Highlander, tunahitaji wachambuzi wa uchumi. Tunahitaji tafiti, wachambuzi, waandishi n.k. Ila kutokana na ushabiki tunaelekeza nguvu zote kwenye TAWLA, TAMWA, Elimu, n.k na kusahau kabisa masuala mengine ya msingi. Wachumi wa vyuo vikuu, je mpo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…