Inflation, ongezeko la bei katika bidhaa

Inflation, ongezeko la bei katika bidhaa

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
INFLATION

Hiki ni kipindi ambacho thamani ya pesa inashuka kutokana na bei ya bidhaa ambazo ni muhimu (necessity goods) kupanda.


What-is-inflation.jpeg

Vyanzo vya mfumuko wa bei.

1. Ongezeko la ajira
Kuongezeka kwa ajira kutasaidia watu kuweza kujitegemea na kuweza kupata kipato. Kipato kikiwa kikubwa basi itasaidia wewe kuweza kununua vitu ambavyo ulikuwa hauna uwezo wakukinunua kabla, na kama mnavyokumbuka when demand increase and supply is constant , it will cause increase in price.

2. Sheria za nchi
Kama serikali ikiweka vikwazo katika uzalishaji wa bidhaa flani, basi hii itafanya kuwe na mfumuko wa bei.

Mfano: Ruzuku zinazotolewa na serikali kwa wakulima zikiacha kutolewa zitasababisha bidhaa za kilimo kupanda bei.

3. Nchi ikiwa na madeni
Nchi ikiwa na madeni mara nyingi itaongeza kodi kwa wafanya biashara ili nchi iweze kulipa madeni yake, kodi zikiongezeka wafanyabiashara wataongeza bei ili waweze kulipa kodi na kuendelea na biashara bila kula hasara.



4. Misimu
Kuna bidhaa ambazo ni za msimu, kwahiyo kama sio msimu wake ni lazima zitapanda bei.

5. Ongezeko la thamani ya fedha za kigeni

Mfano: USD ikipanda, hii itafanya bidhaa zinazoletwa nchini kutoka nchi nyengine kuwa na gharama kubwa, kwahiyo bei ya hizo bidhaa lazima ipande.

Karibuni sana kutoa maoni kuhusu kulipuka kwa bei.

#uchumi #inflationInflation, Ong
 
Hebu nielimishe kwa hili: wakati Mkapa akiwa Rais alilipa sana madeni lakini uchumi wetu ulikua na bei za vitu zilishuka sana. Mfano, sukari 500/kg, bati ft 10, 4800/, petrol 0. 5k/l, cement 4k/bag.
Bei za bidhaa Dar es Salaam ni kubwa tofauti na vijijini na ndio kwenye maendeleo, inflation kwa kiasi ni nzuri kwa maendeleo kwasababu inasaidia pia misharaha kuongezeka, wenye hela watatamani kuongeza uzalishaji na kuwekeza kwasababu bei za bidhaa zimepanda , wakifungua mabiashara basi wataajiri watu, kwahiyo hela inakuwepo kwenye mzunguko.
 
Kwa tz nikiangia suala la ongezeko la ajira bado.watubweng ni jobless haswa vijana.
tz labda tuangalie sana kwenye cost push inflation.my opinion
 
Vita vinavyoendelea huko Ukraine-Russia tayari vimesababisha bei ya mafuta kupanda bei, hii itapelekea inflation ya bidhaa karibu zote.
 
Back
Top Bottom