Ingekuwaje kama JF wangefuta POST zote tukaanza na moja 2018..?

Mgodo visa

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Posts
3,590
Reaction score
3,632
Habari zenu JF members na wale watumiaji wa kawaida wa Wavuti hii.

Baada ya kuaga mwaka wa 2017 kwa furaha na wengine wakiwa na Frustration kibao pamoja na Stress baada ya mambo yao/yetu kwenda ndivyo sivyo (maisha hayana budi kuendelea)

Tumshukuru Mungu kuingia mwaka mpya wa 2018.

Tumshukuru pia Jalali (Muweza wa yote) kumuwezesha C.E.O M.Melo kwa Moyo wake wa ujasiri (pamoja na magumu anayo pitia) kutupa Jukwaa ambalo humu tunakuwa huru kushauri, kukosoa, kutania, kupongeza mwisho kabisa kutoa Povu (pale unapo shindwa kujizuia) pongezi kwa Ndugu yetu Melo, endelea kubeba Dhamana juu yetu.

Kama binaadamu, kuna wakati tunahitaji kufuta kumbukumbu Mbaya na kusahau, ili kuweza kuanza Maisha mapya na yule alie kukosea.

Kuna kumbukumbu nyingi katika Wavuti/Seva ya JF (Nzuri na Mbaya)
Hizi zinabaki kama kumbukumbu yaweza kuwa kwa watoto wetu (vizazi na vizazi)
Humu kuna chungu na tamu.
Chafu na safi.

Kuna Magonjwa na tiba zake pia.

Najaribu kuwaza, ingekuwaje..! Ni furaha ama majonzi kiasi gani (inge/yange wapata baadhi) kama mtandao huu wa JF ungefuta kumbukumbu zote katika Server yake na kufungua ukurasa mpya.

Ni jambo linalowezekana, pia ni jambo linalo hitaji Ukichaa katika maamuzi.

Heri ya Mwaka mpya.
 
Kuna wanaotafuta me/ke, hawajaleta mlejesho.

Kuna waliotabili wanasubili yatokee nk .

Wewe unafikili zikifutwa itakuawaje!!
 
Kuna wanaotafuta me/ke, hawajaleta mlejesho.

Kuna waliotabili wanasubili yatokee nk .

Wewe unafikili zikifutwa itakuawaje!!
ID za wale/yule unae muhitaji kwa Mgegedo zinabakia humu kama kawaida..!
 
Heri ya mwaka mpya Mkuu
Na wewe pia Dada yangu, najua/natambua ushirika na uwepo wako JF
Najua nawe ni moja miongoni mwa Wanachama SUPERIOR ukiwa na RUNDO la Post humu..!

Usihofu kumbukumbu zako kupotea, nimeleta UZI huu, nipate kujua wangapi wana HANG OVER kama yangu.
 
Kufukua makabur kuna raha yake......
Elezea kidogo raha yake, maana sioni umuhimu wakd wake zaidi ya kutonesha KIDONDA kilicho anza kukauka, na kama si kujiumiza Moyo wako, basi utauumiza wa mwenzio...!

Jaribu kidogo kueleza kwa kufikiri, itatusaidia kuelewa unacho maanisha..
 
Elezea kidogo raha yake, maana sioni umuhimu wakd wake zaidi ya kutonesha KIDONDA kilicho anza kukauka, na kama si kujiumiza Moyo wako, basi utauumiza wa mwenzio...!

Jaribu kidogo kueleza kwa kufikiri, itatusaidia kuelewa unacho maanisha..
Inakomesha wale waongo waongo wasio na kumbukumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…