Mzee mwenzangu Bishanga, kwa uzee huu nilionao, nimekuwa nikiwaza na kujiuliza maswali mengi yenye utata, kwa kuwa katika jamii yetu, haya yapo, ndio maana najaribu kuwashirikisha wana JF wenzangu ili kupata changamoto zao. nafurahi kwamba napata majibu mengi yenye kuelimish, na ninaamini hata wasomaji watakuwa wamejifunza jambo pale watakapojikuta wamepata mtihani unaofanana na yale ninayouliza humu.
Nimefarijika sana baada ya my Daughter Lizzy kuweka thread ya kuelimisha juu ya utegemezi (
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/197043-utegemezi.html) likiwa ni wazo lililotokana na thread hii. hii inathibitisha kwamba yale ninayouliza humu huibua mengi ambayo hatuyajui na hapo ndipo tunapopata somo..............