Injiania Hersi Mwambie Senzo Kuwa Anatumia Mbinu za Kizamani Kupoteza Maboya Wapinzani.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Binafsi sioni tija ya kutumia mbinu/propaganda hizi ili kuwaondoa mchezoni Rivers UTD. Naziona kama ni propaganda za kizamani sana.

Cha kushangaza mmeamua kutumia midomo ya upande wa pili ili ku-PUSH propaganda zenu ziwafikie Rivers UTD. Mmegundua dhahiri kuwa ni rahisi sana habari kama hizi kuwafikia Rivers UTD ili wabweteke wakitambua kuwa wachezaji 2 (Djuma & Aucho) ambao pia ni mhimili wa Team hawato kuwapo kwenye mchezo wa kirafiki.

Narudia tena hizi ni mbinu za kizamani sana.

Mmezitengeneza hizi propaganda mkijua rasmi kuna kundi la watu ni wavivu kutumia "deribarative mind" kufikiri kwa kina.

Ninadhani ni wakati wa kumakinika katika kuiandaa Timu kuliko kupanga Propaganda kama hizi, Nimekumbuka kipindi kile tunapeleka waarabu CCM Kirumba mwanza baada ya kugundua kuwa hatukuwa tumejiandaa vyema.

Sidhani hata wao Rivers UTD watazichukulia hizi habari kama zilivyo ili hali kila mtu aliye AVEC TOWN anamuona Djuma akifanya mazoezi ya kimkakati (Strategic Drills) ambayo yanalenga kuwakabili Rivers UTD. Sasa kwanini ajumuishwe kwenye strategic drills ili hali hatocheza mechi dhidi ya Rivers UTD? Mnadhani watu hawajui kuwa Coach Nabi si miongoni mwa aina ya wale makocha ambao mnaweza kuwaendesha?

Kuhusu Aucho. Mnadhani hata wao wavuvi wa kinaigeria hawatambua kuwa Aucho alipo maliza mkataba wake na Misr El Makkasa SC coach Mohamed Abdel-Galil hakutaka kuendelea kuwa na Aucho? Kwanini mzushe kuwa ITC yake ndiyo itamkwamisha?

Leo nimepata nafasi ya kuzungumza na wakala wa Djuma (Bw Mukandila) ambaye pia ni wakala wa Mukoko na Tuisila. Amekanusha mazima habari za propaganda zenu kumhusu Djuma. Pia nikaamua kumvutia waya ndugu Fekir Behladini ambaye ni Kit Manager wa Misr El Makkasa naye amekanusha kabisa hizo taarifa za kuhusu Khalid Aucho. Kwa mujibu wake anametabaisha kuwa ITC ta Aucho ili toka tu mara alipo amua kuto-kuEXTEND mkataba wake kutokana na tofauti ya mchezaji na Kocha.

Hizi ni mbinu za kizamani wala hazitokuwa na msaada katika Ushindi wetu siku ya jumapili. Tutawachapa kwa sababu tunayo NIA ya kuwachapa. Tutawakung'uta kwasababu tunayo SABABU ya kuwakung'uta.

Shubamiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit zenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…