Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Yanga ni wapinzani wangu na siwapendi, nimefurahi sana kuondolewa leo maana tusingekaa mjini, maneno ya shombo ya zungu pori, maneno ya hovyo ya Ally Kamwe yangetuchoma sana sisi watu wa Simba.
Eti wangeshinda leo wangekuwa nafasi ya 5, ujinga kabisa.Ila nnao uhakika kuwa Yanga wamepigana pini wenyewe kwa wenyewe, kuna kamchezo fulani ambako Simba tunao huo ujinga leo Yanga wamefanyiana wenyewe kwa wenyewe.
Injinia ni mjeuri sana, anajiona ana akili kuliko wenzake, anajiona bila wakongwe pale jangwani timu inaweza kupata mafanikio, yaani kiufupi kuna watu ndani ya timu hiyo wamemuumiza injinia leo ili ajue kuwa timu hiyo ina wenyewe na aache kiburi.
Soma Pia: FT: Yanga 0-0 MC Alger | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.01.2025
Wahuni ndani ya timu hiyo walifanya kazi moja tu, kuwapiga pini wachezaji wao, pini hiyo ilipigwa kwa wachezaji wote, wachezee mpira weeeee lakini goli halipo, yanga wamecheza mpira mkubwa sana, wameshinda golini kwa MC Algers lakini pini iliyowekwa ilikuwa sio ya kawaida, wajanja wanaotaka kumuonyesha injinia waliweka mkakati siku nyingi tu kuwa lazima wamkwamishe maana hawaoni faida ya kuendelea kuwa naye, sasa hivi wanamfanyia undava tu.
Nakushauri Injinia ishi nao vizuri uliowakuta ndani ya Yanga, vinginevyo utaondoka kama alivyoondoka Lloyd Nchunga.