Injinia Hersi Said: Timu za Simba na Yanga zinaendeshwa kwa hasara miaka mingi

Mbona anaanza kuchoka mapema hivi!!?
Ndio ligi inaanza hatutaki lawama mbele ya safari.

Hebu tuongee ukweli sasa.
Matangazo aka mabango yaliyo kwenye jezi yanaoita kwenye luninga ya Azam 90min. Maana yake garama ya kutangaza bidhaa yako umetumia TV kwa njia rahisi.

Let say gharama ya kutangaza advert AZAM ni 500,000 kwa dakika.
Maana yake 90min 45,000,000

Piga hesabu 45,000,000 x mechi 30

It means 1.3b

Sasa tuseme umeuza jezi 200,000
Mabango yakiyopo kwenye jezi yanazunguka mpaka vijijini ndani ndani kabisa.

Tuseme bei ya kawaida ya tangazo kwa kila T shirt ni 10,000 kwa mwezi
Maana yake 10,000×12×200,000
Maana yake 24 billion.

Yaaan pesa aliyotumia MO kuilipa simba ni operational costs za mwaka mmoja tu.

Waache uongo sisi siyo wajinga.
 
Kwakua MO ni muongo, jezi moja ya Simba Ina bidhaa za MO Kama Tano na kila bidhaa inatakiwa iwe na mkatabawake Sasa inakuaje mapato ya timu Mwaka yashindwe kuendesha Klabu wakati Kuna wadhamiini wengine Kama Azam na Mo
Mkweli ni GSM Tu.
Tumeisha wazoea.
 


Kwahiyo Mo analipa bilioni moja kwa matangazo yake yote?
Unamjua Mo vizuri??Alipe bilioni kwa Simba kutangaza bidhaa zake?

Mo?
 

Ukiwaambia pisha mdhamini mwingine hawataki
 
Basi waondoeni wawekezaji timu ijiendeshe Kwa hayo matangazo yake ambao mnayo yapigia hesabu kama yanafaida hizo.

Yanga alivyoondoka Manji kila kukicha mlikuwa mnampigia magoti arudi kuwadhamini.
Kwani hamkuwa na matangazo ya kuyaweka kwenye jezi na kuwaingizia pesa za kuendesha timu ?

Wawekezaji wa Ligi yetu wengi wanazifadhiri timu Kwa mapemzi Yao Tu Kwa timu husika.
Ndio maana GSM hawezi kuifadhiri Simba hata iweje.

Wekeni basi matangazo yenu muendeshe vilabu.

Tatizo la washabiki wengi wanajua kuongea Tu.
MO Alisha weka wazi kuwa anaifadhiri Simba Kwa mapenzi yake binafsi Tu
Kama ameweza kuanzisha MO Foundation ambayo ni huduma Tu ya kurudisha pesa Kwa jamii na hapati faida yoyote.
Vipi ashindwe kuifadhi Simba Kwa lengo lilelile la kurudisha faida Kwa wananchi
Nyie kazi yenu ni kupiga soga Tu na kudakua.
Wekeni matangazo yenu muzihudumie hizo timu.
Lopolopo nyingii unafikiri mna uwezo wa kumlipa hata mshahara wa mchezaji mmoja Tu.
 
HAWAWEZI KUKUBALI ABADAN

Mfanyabiashara yeyote anataka cost(expenditure) minimization.
Kutumia team kutangaza bidhaa ni njia rahisi na cheap.
Halafu wengine wananunua bidhaa kwa ushabiki tu.

Soda za Mo zinakaribia kumpita Azam..
Au labda zishampita
Kabla hajatangaza Simba alikuwa hauzi hata nusu ya wanavyouza Azam..
 

Nyinyi ndo watu wenye akili nyepesi mno
Mnarubuniwa na maneno mepesi bila kufanya utafiti..

Hiyo Mo foundation we unajua matumizi yake yote?Kwanza kwanini Non profit Foundation itangazwe kwenye jezi?Umewahi jiuliza?

Je foundation ni Mali ya mtu?
Mo foundation ni Mali ya Mo?
Manake Nyerere foundation sio mali ya familia ya Nyerere...
Foundation hazilipi kodi...
Mo anajua anachokifanya na hiyo Mo foundation...
 
Hao ma-fans ambao wanashindwa kulipa elfu 5 kwenda Uwanjani halafu wanasikiliza kwenye redio au Kibanda Umiza kwa Jero?

Au mashabiki ambao wanashindwa kuchangia timu yao kupitia jersey kwa elfu 35, na badala yake wanaenda K/koo kununua za buku tatu tatu?

Au unazungumzia mashabiki gani?
 
Ubongo kisoda utajulia wapi haya mambo.
Kwenye biblia imeandikwa:-

Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.

Mithali 27:22
 
Kwahiyo Mo analipa bilioni moja kwa matangazo yake yote?
Unamjua Mo vizuri??Alipe bilioni kwa Simba kutangaza bidhaa zake?

Mo?
Hapana sikumanisha kama unavyosema wewe. Nilikuwa namfanyia hesabu nyepesi mtu hapa, maana kadai Mo kaweka matangazo matano ndio nikauliza unajua mikataba yake hiko vipi, maana matangazo ya msimu uliopita nadhani MO poa katoa milioni 200. Kwahiyo kama msimu huu ikafanyika hesabu za namna hiyo ni kwamba Simba anaweza kuwa na bilioni moja(I was only clarifying, but I don't think business is done this way) lakini hakuna anayejua mikataba hiko vipi.Kingine bado hiyo bilioni moja ni bajeti ndogo kwa timu kwa msimu mzima
 
Simba na Yanga miaka mingi zilikuwa na shida ya udhamini
Mpira ulidorola.
Leo wadhamni wamejitokeza, Mpira mzuri tunauona, hadi tunafikia kupata uwakilishi WA timu nne kimataifa tunashindana na timu ambazo zina uwekezaji mzuri kama Libya.
Washabiki lazima tuwape muda wawekezaji.
Wameanza kudhamini mpira juzi Tu maneno kibao ya kuwakebehi.
Tunataka kusikia neno moja tu kwamba wanapata faida.
Mbona makampuni ya Migodi kuna wakati yanatangaza hasara na tunakubali.
Home Shopping Center walitanga kupata hasara na ni kawaida ktk biashara.
Katika mpira hatutaki kabisa kusikia muwekezaji kapata hasara.
Hii sio.
 
Ubongo kisoda utajulia wapi haya mambo.
Kwenye biblia imeandikwa:-

Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.

Mithali 27:22
Kisoda vipi tena eleza unachofikiri
Au ndio maana ya Kisoda.
 
Dhamini wewe basi uweke matangazo yako upate faida.
Walipokosekana wadhamini mbona hukujitokeza.
Au timu yako ilikosa matangazo?
Unataka kusikia nyimbo moja tu
Faida Faida Faida.
Tuwekee hapa basi mchanganuo wa hiyo faida
Ili tujue GSM ni Mwongo.
MO ni Mwongo
Wewe ndio Mkweli.
 
Mzee akili zako ni ndogo huwezi elewa tunachoongelea Mzee.
GSM and MO ni wafanyabiashara, tena asili yao ni mwarabu na mhindi.

Hivi kwa akili yako hiyo hao wafanyabiashara wanazipenda saaaana hizo teams!? Kiasi cha kuwekeza kwa hasara!?

WEWE UNGEKUWA MFANYABIASHARA UNGEWEKEZA KWA HASARA.
 
Ukitumia akili bado watakunufaisha.

Wapo wanotafuta hao wa walau kuwataja tu midomoni na hawana.

Wapi utaitaja Simba au Yanga nchi hii Mtu asishtuke?...huo ni mtaji pia.
 
We na akili kubwa yote hiyo bado hufahamu hatua za mahitaji.
Mwanadamu kila anapozidi kupata pesa mahitaji yake yana adilika.
Kasome, Manslow Hierachrchy of Needs ya Abraham Manslow 1943 utaelewa.
Mfanya biashara tajiri inafikia wakati anatumia pesa yake nyingi kutaka fahari tu, na furaha ya moyo wake.
MO alishasema hili
"mi naifadhiri Simba napenda furaha tu"
Matajiri wanaanzisha baadhi miradi ambayo hawapati faida hata chembe, ukiwafuatilia Akina Bill gates, Bezos, Dangote utaelewa vizuri.
Nadharia za Kisomi zinalikubali hili Jambo ndio maana Manslow anaheshimika kitaaluma.
Wewe mwenzetu sijui unatokea wapi

wewe mwenye akili kubwa Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…