Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa, amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), leo tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni siku nne baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha Mawaziri hao tarehe 9, Disemba 2024, Tunguu Zanzibar.
Waziri Bashungwa amemshukuru mtangulizi wake kwa makabidhiano ambayo yatakuwa mwongozo wa kusimamia na kutekeleza majukumu yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi.