JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Tume, Innocent Mungy ameyasema hayo Machi 1, mwaka huu mjini Morogoro wakati akiwasilisha mada ya tafsiri ya taarifa binafsi, amesema mtu anapaswa kuandika kitambulisho chake cha NIDA na sio taarifa za kina ambazo hutumiwa vibaya na watu.
Alitaja taarifa zinazopaswa kulindwa ni jina la ukoo, majina mengine, anwani, historia ya elimu, ajira, NIDA, eneo alilopo (live location), dini, hali ya ndoa, utaifa, kabila , umri, hali ya fedha na afya.
“Kuna watu kazi yao ni kupita sehemu mbalimbali zenye madaftari ya wageni wanawapa fedha kidogo walinzi kisha wanapiga picha kisha wanazitumia kutapeli watu ndio ule ujumbe wa zile fedha tuma kwenye namba hii,”amesema.
Chanzo: Nipashe